Thursday, January 03, 2013

DEMBA BA KUTUA RASMI CHELSEA


Chelsea imesema itamsajili mshambulizi wa Newcastle Demba Ba.
Ba, mwenye umri wa 27, sasa amepewa ruhusa na klabu yake kuzungumza na Chelsea kuhusu uwezekano wa kusajili na klabu hiyo.

Inaaminika kuwa kandarasi ya Demba Ba inaruhusu kuzungumza na vilabu vingine ambayo viko tayari kulipa kitita cha pauni milioni saba kumlipa.

Mshambulizi huyo kutoka Senegal, ambaye alijiunga na Newcastle kutoka klabu ya West Ham mwezi juni mwaka wa 2011, ndiye mchezaji wa pili aliyefunga idadi kubwa ya magoli msimu huu.


Kufikia sasa demba ba amefunga jumla la magoli 13.

Wakati huo huo klabu ya Liverpool imesema kuwa imemsajili mshambulizi wa timu ya taifa ya Uingereza na Chelsea Daniel Sturridge.

Sturridge, mwenye umri wa miaka 23, anaaminika alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu hiyo mwezi uliopita kabla ya mwezi huu wa uhamisho wa wachezaji.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed