
THEO WALCOTT AKISAINI MKATABA MPYA NA ARSENAL PEMBENI YAKE NI KOCHA MKUU WA ARSENAL ARSENE WENGER

THEO WALCOTT AKIPEANA MKONO NA KOCHA WAKE ARSENE WENGER BAADA YA KUSAINI MKATABA MPYA NA ARSENAL

THEO WALCOTT( KATIKATI) AKIPONGEZWA NA WACHEZAJI WENZAKE WA ARSENAL ALEX OXLADE CHAMBERLAIN ( KUSHOTO) NA WOJCIECH SZCZESNY (KULIA)
Hatimaye mshambuliaji wa klabu ya arsenal Theo walcott ameondoa uvumi uliokuwepo kuhusu mustakabali wake wa baadaye na klabu yake ya arsenal kwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.
Mwanzoni mwa mwezi huu mtandao wa Sportsmail ulidhihirisha ukweli kwamba timu ya arsenal iko mbioni kukamilisha mkataba wa mchezaji wa timu ya taifa ya uingereza kwa kumwongezea mshahara hadi kufikia paundi 90,000 kwa wiki na pia angeweza kupata bonasi ya paundi milioni 3.
Baada ya kukamilisha mkataba huo ambao unaisha mwaka 2016 walcott alisema nilikuwa sahihi tangu mwanzo kwamba nataka kubaki katika klabu hii kwa muda mrefu, nina furaha kwa sababu kila kitu kimekwenda viizuri kila mtu ana furaha.
Kitu cha muhimu sasa ni kuthamini mchango wangu na kuisaidia klabu hii kushinda vikombe alisema walcott.
Taarifa hizi zimemaliza vita ya miezi sita kati ya klabu ya arsenal na mchezaji huyo iliyokuwa ikimtaka mchezaji huyo kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.
Theo walcott alikataa ofa ya mwanzo ya Arsenal ya paundi 75,000 kwa wiki wakati washuri wake waliposhinikiza mshahara unaokaribia paundi 100,000 kwa wiki kiasi ambacho Arsenal walikataa kutoa.
Ilifikia wakati Arsenal ilifikiria kumuuza mchezaji huyo katika dirisha la usajili la majira ya joto mpaka meneja wa klabu hiy na mchezaji huyo walipofikia makubaliano na mchezaji huyokukubali kuongeza mkataba na klabu hiyo ya Emirates.
Mchezaji huyo alikuwa ameanza kuzivutia timu za manchester city, Manchester united na liverpool ambazo zilikuwa na mpango wa kumsajili mchezaji huyo mwishoni mwa msimu akiwa mchezaji huru.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed