Tuesday, February 05, 2013

CRISTIANO RONALDO APANIA KUIFUNGA UNITED

RONALDO AKIWA KATIKA HARAKATI ZAKE UWANJANI
Mchezaji wa Timu ya Real madrid cristiano Ronaldo amemwagia sifa kocha wa klabu ya Manchester united Sir Alex Ferguson kwa kumfundisha mbinu mbalimbali katika medani ya soka lakini amesisitiza kwamba ataweka shukrani zake zote pembeni kwa kuitupa nje ya mashindano ya klabu bingwa barani ulaya klabu ya Manchester United.
Mchezaji huyo mahili wa klabu ya Real madrid ambaye amefunga mabao 179 katika michezo 178 aliyoichezea klabu yake ya madrid tangu ajiunge nayo kutoka manchester united mwaka 2009 anaamini atakuwa mtu muhimu sana katika klabu yake katika timu 16 zilizobaki wakati atakaporudi Old Trafford katika pambano la kwanza litakalopigwa jumatano ijayo.

Mchezaji huyo wa nafasi ya ushambuliaji kutoka Ureno anatarajia kung'aa katika pambano hilo akiamini kwamba mambo yatakuwa mazuri kwa upande wake.

Akiiongelea Real madrid Ronaldo amesema wanayo timu nzuri inayoweza kutoa upinzani kwa timu yoyote ile lakini cha msingi ni kuonyesha uwezo wao ndani ya uwanja, na kwa upande wa manchester united Ronaldo amesema Manchester united ni klabu bora kabisa katika mashindano hayo na ni timu yenye umoja na mshikamano na imedhihirisha hilo kwa miaka mingi.

Akiongea maneno hayo Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 sasa amesema hana nia ya kumuumiza mtu yeyote katika klabu ya manchester united na kwamba anaheshimu klabu hiyo ambayo ilimpatia umaarufu na heshima kubwa baada ya manchester united kumnunua kutoka katika klabu ya Sporting Club De Portugal mwaka 2003 kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 15.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed