
KOCHA wa Tottenham ANDRE VILLAS BOAS amewahakikishia mashabiki wa klabu ya Tottenham kwamba Emmanuel Adebayor atakuwa tayari kwa pambano la jumamosi ijayo dhidi ya Newcastle.
Adebayor alikuwa anaiwakilisha timu yake ya taifa ya Togo katika mashindano ya kombe la mataifa ya afrika na hakuwepo tangu tarehe 12 mwezi wa janauri.
Timu ya taifa ya Togo iliondoshwa katika mashindano hayo kwa kuchapwa na Burkinafaso katika pambano lililopigwa jumapili iliyopita na mchezaji huyo yupo mbioni kurudi katika mazoezi ya kikosi cha Tottenham inayojiandaa kwa pambano lake dhidi ya Newcastle siku ya jumamosi.
Mchezaji huyo alikuwa amepewa mapumziko baada ya kuondolewa katika mashindano ya afrika lakini kuumia kwa mchezaji wa nafasi ya ushambuliaji ya Tottenham Jermain Defoe kumemfanya mchezaji huyo kurudi mapema ili kuweza kuongeza nguvu katika kikosi hicho.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed