Wednesday, February 27, 2013

MATOKEO MECHI YA JANA COPA DEL REY

BARCELONA 1 REAL MADRID 3(Agg 2-4) CRISTIANO RONALDO AIPELEKA REAL MADRID FAINALI YA COPA DEL REY
Cynical: Ronaldo was brought down by Gerard Pique in the penalty area in the 13th minute
GERALD PIQUE AKIMWANGUSHA RONALDO KATIKA ENEO LA HATARI NA KUSABABISHA PENALTI ILIYOFUNGWA NA RONALDO
Lead: Ronaldo sent Jose Manuel Pinto the wrong way to open the scoring from the spot
RONALDO AKIFUNGA KWA PENALTI
Star: Cristiano Ronaldo scored two goals as Real Madrid beat Barcelona 3-1 at the Nou Camp
CRISTIAN RONALDO AKISHANGILIA GOLI LA KWANZA LA REAL MADRID
Gap: Ronaldo followed up Sami Khedira's effort to double Madrid's lead in the second halfCRISTIANO RONALDO AKIIFUNGIA REAL MADRID BAO LA PILI
Gap: Ronaldo followed up Sami Khedira's effort to double Madrid's lead in the second half
RONALDO AKISHANGILIA
Cruising: Raphael Varane rose highest to head home from a corner and put Real 3-0 upRAPHAEL VARANE AKIRUKA HEWANI KUIFUNGIA REAL MADRID BAO LA TATU
Delight: Varane celebrated his goal with manager Jose Mourinho 
RAPHAEL VARANE AKISHANGILIA GOLI LA TATU
Delight: Varane celebrated his goal with manager Jose Mourinho
RAPHAEL AKIMKUMBATIA KOCHA WAKE JOSE MOURINHO
Downbeat: Lionel Messi looked dejected as Madrid cruised past Barcelona
BARCELONA WAKIWA HAWAAMINI KILICHOTOKEA
Lionel Messi
LIONEL MESSI AKIWA HAAMINI BAADA YA KIPIGO
Too little, too late: Jordi Alba scored a late consolation for BarcelonaJORDI ARBA AKISHANGILIA GOLI LA KUSAWAZISHA LA BARCELONA
Opposition: Mourinho talked to Barcelona's assistant coach Jordi Roura before the match
JOSE MOURINHO AKISALIMIANA NA KOCHA MSAIDIZI WA BARCELONA JORDI ROURA
Timu ya soka ya real madrid jana usiku imefanikiwa kutinga fainali ya mashindano ya kombe la mfalme maarufu kama Copa Del Rey kwa kuitandika bila huruma timu ya soka ya Barcelona mabao 3-1 katika pambano lililopigwa katika uwanja wa Camp Nou.

Alikuwa ni mshambuliaji hatari wa klabu ya Real madrid Cristiano Ronaldo ambaye aliamua kujibu shutuma za mashabiki wanaoamini kwamba Lionel Messi ni mchezaji bora Duniani kwa kuweza kupachika bao la kwanza kwa njia ya mkwaju wa penalti katika dakika ya 13 ya mchezo baada ya kufanyiwa rafu na Gerald pique katika eneo la hatari kwa kufunga penalti safi akimwasha kipa wa Barcelona Manuel Pinto hana la kufanya.

Katika dakika ya 57 Cristiano Ronaldo tena aliwanyanyua mashabiki wa Real madrid kwa kuweza kupachika bao la pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Angel Di Maria ambaye alimlamba chenga ya mwili Cares Puyol na kutumia akili nyingi kuipasua ngome ya Barcelona.

Karamu ya magoli ya Real madrid ilikamilishwa na mchezaji chipukizi wa nafasi ya ulinzi wa kati kutoka ufaransa Raphael varane aliporuka juu zaidi na kufunga goli safi katika dakika ya 69 kufuatia mpira wa kona.

Pambano la jana lilishuhudiwa na kocha wa manchester united Sir Alex Ferguson ambaye alikuwepo katika uwanja wa Camp Nou kuwashuhudia Real madrid wakiitandika Barcelona hiin ni moja kati ya mikakati ya kocha huyo kuhakikisha anawamaliza Real madrid katika pambano la marudiano litakalopigwa wiki ijayo katika uwanja wa Old Trafford katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya.

Ulikuwa ni usiku mzuri sana kwa kocha wa Real madrid Jose Mourinho katika jiji la Barcelona tangu alipotua hispania na klabu ya Inter Milan ya Italia na kuchukua ubingwa wa klabu bingwa barani ulaya mbele ya kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola. Kukosekana kwa kocha Pep Guardiola na kocha wa sasa Tito Vilanova kumeanza kuonyesha tofauti kubwa katika klabu ya Barcelona.

Kwa kufanikiwa kufunga bao mbili katika uwanja wa Camp Nou Cristiano Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza kuweza kufunga katika mechi sita mfululizo za ugenini za mahasimu hao wa hispania maarufu kama Clasicos.

Katika pambano hilo mchezaji nambari moja kwa ubora Duniani na anayeongoja kwa kupachika mabao mengi katika ligi ya uhispania Lionel Messi alionekana si chochote mbele ya Mchezaji kinda wa nafasi ya ulinzi wa kati mwenye umri wa miaka 19kutoka ufaransa Raphael Varane ambaye aliweza kumdhibiti mchezaji huyo na kushindwa kabisa kufurukuta na kuleta madhara kama ilivyo kawaida yake katika mapambano mengine yaliyopita.

VIKOSI VILIPANGWA KAMA IFUATAVYO
Barcelona: Pinto, Alves, Pique, Puyol, Jordi Alba, Sergio, Xavi (Alcantara 74), Cesc (Villa 60), Pedro (Tello 71), Iniesta, Messi.

Subs not used: Valdes, Mascherano, Adriano, Song.

Goals: Alba 89.

Real Madrid: Diego Lopez, Varane, Ramos, Coentrao, Khedira, Cristiano Ronaldo, Ozil (Pepe 79), Xabi Alonso (Essien 84), Arbeloa, Higuain (Callejon 70), Di Maria.

Subs not used: Adan,Kaka, Benzema, Modric.

Goals: Ronaldo 13, 57, Varane 68.

Att: 90,002.

Referee: Undiano Mallenco.



No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed