
Kikosi cha Young Africans kilichoanza dhidi ya Azam FC
Mabingwa wa kombe la Kagame timu Young Africans leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa timu ya Azam FC kwa bao 1-0, katika mchezo uliofanyika jioni hii katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kwa matokeo haya ya leo Young Africans imezidi kujikita kileleni kwa kufikisha pointi 39 na mabao 34 ya kufunga, timu iliingia uwanjani kwa ajili ya kusaka pointi 3 muhimu ambazo imefanikiwa kuzipata na kuendeleza ubabe dhidi ya waoka mikate wa Bakhresa.
Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi, na katika dakika 15 za kwanza mshambuliaji wake Jerson Tegete alikosa nafasi za kufunga mabao ya wazi ya mapema, kufuatia kutokua makini katika umaliziaji kufuatia kubakia yeye peke yake ni mlinda mlango wa Azam Mwadini Ally.
Yanga iliendela kuutawala mchezo na hasa sehemu ya kiungo, ambapo Haruna Niyonzima, Athumani Idd Chuji, Frank Domayo waliweza kuitawala sehemu hiyo ya katikati hali iliyopelekea wachezaji wa Azam FCkuhangaika kuumiliki mpira.
Dakika ya 31, Haruna Niyonzima aliipatia Young Africans bao la kwanza na la ushindi baada ya kumchambua mlinda mlango wa Azam Mwadini Ally kufuatia migongeo kati yake na Jerson tegete na Hamis Kiiza kabla ya Niyonzima kuukwamisha mpira wavuni kwa ufundi wa hali ya juu.
Dakika ya 42, Jerson Tegete tena alishindwa kuipatia Young Africans bao la pili tena baada ya kushindwa kumalizia pasi safi ya Hamis Kiiza aliyewatoka walinzi wa Azam FC na kumpasia Tegete ambaye alipiga shuti hafiifu likiodakwa na Mwadini Ally wa Azam FC.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Young Africans 2-0 African Lyon.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Azam ilifanya mabadiliko ili kuongeza nguvu na kuona kama itaweza kupata bao la kusawazisha lakini mabadiliko hayo hayakuwa na tija yoyote kwani umakini wa walinzi wa Yanga na mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez' ulikuwa kikwazo kwao kupata bao lolote.
Jerson Tegete alikuwamisha mpira wavuni dakika ya 61 kufuatia pasi safi ya kiungo Saimon Msuva lakini mwamuzi wa mchezo alilikataa bao hilo kwa madai kuwa mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga.
Yanga ilifanya mabadiliko ya kuwaingiza Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi kuchukua nafasi za Hamis Kiiza na Jerson Tegete mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya ushambuliaji kwa timu ya Yanga na walinzi wa Azam kuwa na kazi ya ziada kuwadhibiti.
Mwamuzi Hashim Abdallah aliiinyima Yanga penati mbili kufuatia mshambuliaji Didier Kavumbagu kuchezewa madhambi na mlinda mlango wa Azam Mwadini Ally wakati akielekea kufunga lakini mwamuzi huyo alikaa kimya na kuashiria Kavumbagu hakuchezewa madhambi dakika ya 70, 82
Mpaka dakika 90 za mwamuzi Hashim Abdall zinamalizika , Young Africana 1- 0 Azam FC.
Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema amefurahishwa kwa ushindi na kukipongeza kikosi chake kwa kupata kwa ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza timu ilicheza vizuri na kumiliki mchezo hali iliyopelekea kupata bao hilo moja na la ushindi, pongezi kwa kiungo Haruna Niyonzima kwa kufunga bao hilo kwa ustadi wa hali ya juu.
Azam ni timu nzuri lakini nilishasema toka awali kuwa sisi ni wazuri na bora kuliko wao, hivyo nilitarajia timu itaibuka na ushindi katika mchezo wa leo na ndio matokeo yaliyotokea kwa timu yangu kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Baada ya mchezo huu wa leo kikosi cha Young Africans kesho kitakua mapumziko na kitaendelea na mazoezi tena siku ya jumatatu asubuhi katika uwanja wa mabatini Kijitonyama ikiwa ni maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya timu ya Kagera Sugar siku ya jumatano katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Mbuyu Twite, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva, 8.Frank Domayo, 9.Jerson Tegete/Didier Kavumbagu 10.Hamis Kiiza/Sadi Bahanuzi, 11.Haruna Niyonzima
Azam FC: 1.Mwadini Ally, 2.Michael Bolou, 3.Waziri Salum, 4.David Mwantika, 5.Joackins Atudo, 6.Ibrahim Mwaipopo/Himid Mao, 7.Khamis Mcha/Seif Abdallha, 8.Salum Abubakar, 9.John Boko, 10.Humphrey Mieno, 11.Kipre Tchethce
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed