
Kaizer chiefs wameendelea kubaki juu ya msimamo wa ligi ya nchini afrika ya kusini kwa pointi tano juu ya mahasimu wao Orlando pirates baada ya hapo jana kutoka sare ya bila kufungana.
Pambano la watani wa jadi hao lilipigwa jana nchini afrika ya kusini katika uwanja wa FNB uliopo johanesburg na kushuhudia miamba hiyo ikitoka nje bila kufungana.
Kaizer chiefs ambao wako juu ya msimamo wa ligi hiyo walikuwa wakijaribu kuongeza tofauti ya pointi kati yake na Orlando pirates lakini timu hiyo maarufu kama Amakhosi walishindwa kuwafunga wapinzani wao hao.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed