
RONALDO AKIIANDIKIA REAL BAO LA PILI
RONALDO AKINYOSHA MIKONO JUU BAADA YA KUIFUNGIA REAL MADRID BAO LA PILI


LUCA MODRIC AKIIFUNGIA REAL MADRID BAO LA KWANZA


LUIS NANI WA MANCHESTER UNITED AKIONYESHWA KADI NYEKUNDU BAADA YA KUCHEZA RAFU

DANNY WELBECK AKISABABISHA GOLI LA KWANZA LA UNITED
Timu ya manchester united jana usiku ilijikuta ikitupwa nje ya mashindano ya klabu bingwa barani ulaya maarufu kama UEFA Champions league kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 katika uwanja wa nyumbani wa Old trafford.
Manchester united ambayo ilianza kwa kasi pambano la jana ilifanikiwa kupata bao lake la kwanza katika dakika ya 48 baada ya kutokea purukushani katika lango la madrid na Sergio Ramos kujikuta akijifunga mwenyewe na kuipatia united bao la kwanza.
Katika dakika ya 57 ya mchezo mchezaji wa manchester united Luis Nani alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kuonyesha mchezo mbaya dhidi ya real madrid, kutolewa kwa Luis nani kuliifanya safu ya ushambuliaji ya manchester united kuanza kupwaya na ndipo kocha wa real madrid Jose Mourinho akatumia mwanya huo kwa kumtoa Arbeloa na nafasi yake kuchuliwa na Luca Modric.
Mabao ya Real Madrid yaliwekwa nyavuni na Luca modric aliyefunga kwa kupiga mpira wa mbali uliomshinda kipa wa manchester united David Degea katika dakika ya 67 kabla ya Cristian Ronaldo kumalizia bao la pili katika dakika ya 69.
Timu ya Manchester united itabidi ijilaumu yenyewe kwa kuweza kuruhusu mabao mawili katika muda wa dakika mbili ambapo Real madrid waliweza kuzitumia na atimaye kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
WACHEZAJI WA AKIBA: Lindegaard, Evans, Hernandez, Kagawa.
KADI YA NJANO: Evra, Carrick
KADI NYEKUNDU: Nani 57.
WAFUNGAJI: Ramos (OG) 48.
REAL MADRID: Diego Lopez, Arbeloa (Modric 59), Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Khedira, Alonso, Di Maria (Kaka 42), Ozil (Pepe 71), Ronaldo, Higuain.
WACHEZAJI WA AKIBA: Adan, Benzema, Albiol, Callejon.
KADI YA NJANO: Arbeloa, Pepe
WAFUNGAJI: Modric 67, Ronaldo 69.
Referee: Cuneyt Cakir (Turkey)
WATAZAMAJI: 74,959
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed