Sunday, March 03, 2013

REAL MADRID YAIZIMA BARCELONA KWA MARA YA PILI MFULULIZO YAIPIGA BAO 2-1

SERGIO RAMOS AKISHANGILIA PAMOJA NA LUCA MODRIC BAADA YA KUIFUNGIA REAL BAO LA PILI KATIKA DAKIKA YA 81
Delight: The Real Madrid fans celebrate a second win over Barcelona in five days
Equaliser: Lionel Messi levelled the scores for Barcelona on 17 minutes with his 50th goal of the season
LIONEL MESSI AKIWA NA FURAHA BAADA YA KUISAWAZISHIA BARCELONA KATIKA DAKIKA YA 17 YA MCHEZO
Karim Benzema celebrates scoring the opening goal
KARIM BENZEMA AKISHANGILIA BAADA YA KUIFUNGIA REAL MADRID BAO LA KWANZA KATIKA DAKIKA YA 5
Timu ya soka ya Barcelona imejikuta katika wakati mgumu baada ya jana jioni kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa mahasimu wao wa jiji la madrid timu ya real madrid ambayo inanolewa na kocha mreno Jose Mourinho maarufu kama the " The only one".

magoli ya Real madrid katika pambano la jana yalifungwa na Karim benzema katika dakika ya 5 ya mchezo kabla ya Lionel Messi kusawazisha katika dakika ya 17 na bao la pili lilipatikana katika dakika ya 81 ya mchezo lililowekwa nyavuni na Sergio Ramos.

Kocha wa Real madrid Jose Mourinho alichezesha kikosi tofauti na kile ambacho kilifanya mauaji katika kombe la mfalme maarufu kama "Copa Del Rey" kwa kuwaanzisha kaka, Benzema na Luka Modric na kuwaweka katika benchi wachezaji wake maarufu Cristiano ronaldo, Sami khedira na Arbeloa ambao walikuja kuingia uwanjani baadaye katika dakika ya 57(Khedira) aliyechukua nafasi ya Benzema , dk.59 (Ronaldo) aliyechukua nafasi ya Kaka na dk.70 (Arbeloa) aliyechukua nafasi ya Coentrao

VIKOSI
Real Madrid: Lopez; Ramos, Varane, Pepe, Coentrao (Arbeloa 70); Essien, Modric; Callejon, Kaka (Ronaldo 59), Morata; Benzema (Khedira 57)
Substitutes: Adan, Ozil, Carvalho, Higuain, Arbeloa
Scorer: Benzema 5, Ramos 81
Booked: Ramos, Coentrao, Morata

Barcelona: Valdes; Alba, Piqué, Mascherano, Alves; Busquets, Thiago (Tello 87), Iniesta; Villa (Alexis 67), Messi, Pedro (Adriano 76)
Substitutes: Pinto, Puyol, Song, Fabregas
Scorer: Messi 17
Booked: Alba, Pique, Thiago, Messi, Alves
Sent off: Valdes

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed