

RYAN GIGGS
Ryan Giggs amesaini mkataba mpya na manchester united kuendelea kukipiga mpaka mwaka 2014
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 sasa amemwaga wino kwenye karatasi za manchester united na ataendelea kuwepo klabuni hapo mpaka ifikapo juni 2014 na kukamilisha msimu wa 23 akiwa mchezaji wa klabu moja pekee ya manchester united.
Ryan Giggs ambaye ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Wales alianza maisha yake ya soka klabu ya manchester united mwaka 1991 na kufanikiwa kufunga magoli 168 katika michezo 931 aliyoichezea klabu hiyo.
Akiongea na BBC mchezaji huyo amesema anajisikia furaha sana na anafurahia maisha yake ya soka katika klabu hiyo na cha zaidi ninajikisikia sehemu ya klabu hii kwa kuwa ninatoa mchango wangu katika timu.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed