
Timu ya soka ya Arsenal inashuka katika dimba la Emirate kupambana na mabingwa wapya wa ligi kuu ya uingereza Manchester united katika pambano ambalo litakuwa maalumu kwa ajili ya bingwa mpya kutambuliwa rasmi na kupewa hadhi ya bingwa mpya wa kikombe cha ligi hiyo yenye wapenzi wengi kabisa duniani.
Pambano hilo litakumbusha kipigo ambacho Arsenal walikipata kutoka kwa manchester katika msimu uliopita wa ligi kwa kukubali kipigo cha mabao 8-2 na pia litakuwa pambano maalumu kwa mchezaji wa Manchester united Robin Van Persie ambaye alikuwa mchezaji wa arsenal msimu uliopita na pia litakuwa pambano ambalo mchezaji huyo ataweza kupata heshima akiwa mmoja wa wachezaji wa kikosi bingwa cha ligi ya uingereza kwa msimu wa 2012/2013.


No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed