
Sergio Ramos akiifungia real bao la pili

Ramos akipiga mpira kufunga bao la pili

Benzema akiifungia real madrid bao la kwanza


Cristiano Ronaldo ameshindwa kabisa kuisaidia real madrid


Gonzalo Higuain akijaribu kupiga mpira bila mafanikio

Lewandowski(kushoto) akigombea mpira na Raphael Varane wa real madrid
Timu ya soka ya Real madrid hapo jana usiku imejikuta ikitupwa nje ya mashindano ya kombe ulaya maarufu kama UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwa kukubali matokeo ya magoli 4-3 kutoka kwa timu ngumu ya Borussia Dortmund ya ujerumani na kufanya ndoto za kocha wa Real madrid za kuwa kocha mwenye mafanikio kwa kuweza kuchukua ubingwa wa ulaya mara tatu akiwa na klabu tatu tofauti kufutika.
Borussia Dortmund ambao katika pambano la wiki iliyopita lililopigwa nchini ujerumani waliweza kuifunga Real madrid mabao 4-1 ambayo yalifungwa na Robert Lewandowisk walikuwa wanahitaji sare ya aina yoyote ili waweze kusonga mbele katika mashindano hayo, na kwa upande wa real madrid wao walikuwa wanahitaji ushindi wa bao 3-0 ili waweze kufuzu kwa hatua ya fainali ya mashindano hayo.
Pambano la jana lilikuwa pambano gumu uku kila timu ikijaribu kutafuta mbinu za kuweza kumfunga mwenzake lakini mambo yalizidi kuwa magumu kwa kikosi cha Jose Mourinho ambao walipoteza nafasi nyingi za wazi kuweza kufunga mabao.
Kipindi cha kwanza kiliisha kwa timu zote mbili kutoka nje bila kufungana lakini katika dakika ya 82 kipindi cha pili Karim benzema aliweza kuipatia Real madrid bao la kwanza na kuzidi kuamsha morali kwa wachezaji wenzake wa real madrid kuweza kupambana na ndipo katika dakika ya 88 Sergio ramos aliweza kuandika bao la pili na kufanya pambano kumalizika kwa magoli 2-0 ambayo yameshindwa kuwavusha real madrid.
Kwa matokeo hayo Real madrid imetupwa nje ya mashindano ya ulaya kwa jumla ya mabao 3-4
VIKOSI
Real Madrid: Diego Lopez, Essien, Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao (Kaka 57), Modric, Alonso (Khedira 67), Di Maria, Ozil, Ronaldo, Higuain (Benzema 57).
Wachezaji wa akiba: Casillas, Pepe, Albiol, Morata.
Kadi za njano: Fabio Coentrao, Higuain, Sergio Ramos, Khedira.
Magoli: Benzema 82, Sergio Ramos 88.
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer, Gundogan, Bender (Felipe Santana 90), Blaszczykowski, Gotze (Grosskreutz 14), Reus, Lewandowski (Kehl 87).
Wachezaji wa akiba: Langerak, Leitner, Sahin, Schieber.
Kadi za njano: Gundogan, Bender, Weidenfeller.
Watazamaji: 76,000
Referee: Howard Webb (England)
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed