Wednesday, May 15, 2013

RIO FERDINAND ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA

RIO FERDINAND
Mlinzi wa Timu ya Taifa ya Uingereza Rio Ferdinand ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa.

Mlinzi huyo wa Manchester united mwenye umri wa miaka 34 sasa ambaye amecheza mechi 81 na timu ya taifa amesema anataka kujikita zaidi katika klabu yake ya manchester united.

Baada ya kukaa na kutafakari nimeona ni wakati muafaka sasa wa kuachia ngazi kutoka katika soka la kimataifa, alisema.

Ferdinand hajaichezea England tangu mwezi june,mwaka 2011 ambapo alishiriki katika pambano la England dhidi ya Switzerland kuwania nafasi ya kufuzu kwa kombe la ulaya( Euro 2012) 

Aliitwa kwa mara nyingine tena na kocha wa sasa wa England Roy Hodgson kwa ajili ya maandalizi ya kombe la dunia brazil katika pambano dhidi ya San marino na Montenegro mwezi machi 2013 lakini alijitoa baadaye kutokana na sababu za kiafya.

Rio Ferdinand amekuwa mhimili imara wa ulinzi katika klabu ya manchester united na ameweza kuisaidia klabu hiyo kurejesha kikombe cha ligi ya uingereza ambacho walikipoteza mwaka jana dhidi ya Manchester city na ametajwa katika timu ya mwaka ya wachezaji walioteuliwa na chama cha mpira wa miguu wa kulipwa cha nchini uingereza.

Najisikia kukaa pembeni ya soka la kimataifa kwa wakati huu na kuwapisha vijana chipukizi waweze kusongesha mbele gurudumu hili kitu ambacho kitanifanya niweze kujikita zaidi katika klabu yangu ya manchester united aliongeza kusema mlinzi huyo wa kati wa zamani wa klabu ya West ham united.

Akiongelea uamuzi wa kustaafu kwa Rio ferdinand kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amesema alipokea taarifa kwa simu kuhusu uamuzi wa Rio Ferdinand kutoka kwa mchezaji huyo.

Ni vizuri kuheshimu mchango wa mchezaji wa aina ya Rio Ferdinand na mafanikio aliyoyapata katika ngazi ya soka la kimataifa akiwa amelitumikia taifa lake kwa miaka 14 akicheza kwa juhudi na maarifa yote.

Naheshimu maamuzi ya Rio Ferdinand kuhusiana na uamuzi wake wa kustaafu baada ya kukaa na kufikiri kwa muda mrefu alisema Hodgson.

Ferdinand anabaki kuwa mchezaji mdogo katika nafasi ya ulinzi kuwahi kuichezea England katika ngazi ya kimataifa baada ya kuonekana kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 19 alipoichezea england dhidi ya Cameroon hiyo ilikuwa mwezi novemba mwaka 1997 pambano lililopigwa katika uwanja wa wembley.

Amecheza katika mashindano ya kombe la dunia matatu mwaka 1998,2002, na mwaka 2006 kabla ya kuondolewa katika dakika za mwisho katika kombe la dunia la mwaka 2010 lililopigwa nchini afrika ya kusini kutokana na tatizo la goti pia alikosa mashindano ya kombe la ulaya mwaka 2003 baada ya kufungiwa miezi 9 na chama cha soka nchini england kutokana na kukwepa vipimo vya kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed