Tuesday, May 14, 2013

ROBERTO MANCINI AFUKUZWA KAZI MANCHESTER CITY

KARAMU YA MWISHO: ROBERTO MANCINI AMEFUKUZWA KUIONGOZA MANCHESTER CITY BAADA YA KUSHINDWA KUTWAA KOMBE LA F.A
MANCINI AKIWA KATIKA UWANJA WA LOFTUS KUJIANDAA NA PAMBANO DHIDI YA READING KABLA YA KUTIMULIWA JANA USIKU
MANCINI AKISINDIKIZWA KUTOKA NJE YA HOTELI BAADA YA KUTIMULIWA
MANCINI AKIWA NA MABEGI YAKE AKIONDOKA KATIKA HOTELI ALIYOKUWA AKIISHI
Utawala wa Roberto Mancini kama kocha wa klabu ya manchester city ulifikia tamati kikatili jana usiku baada ya kocha huyo kutimuliwa na kuonekana kuwa kocha ambaye ameshindwa kufanya vizuri katika klabu ya Manchester city baada ya kushindwa kunyakuwa ubingwa wa F.A.

Roberto Mancini ambaye aliiwezesha klabu ya Manchester city kunyakua ubingwa wa ligi ya uingereza baada ya miaka 47 anategemea kulipwa kitita cha paundi milioni 7, ameambiwa kuwa hatakiwi katika klabu hiyo saa moja baada ya kocha huyo kukiongoza kikosi chake katika mazoezi tayari kwa pambano la leo dhidi ya reading.

Taarifa kutoka klabu ya Manchester city ilisomeka kuwa klabu hiyo inahitaji kufanya mabadiliko kuweza kusonga mbele na kwa sasa inakamilisha mipango ya kuweza kumnyakuwa kocha kutoka chile ambaye anakinoa kikosi cha malaga ya hispania Manuel Pellegrini, taarifa ilizidi kusema kuwa kwa sasa klabu hiyo itakuwa chini ya kocha msaidizi Brian Kidd ambaye ataiongoza timu hiyo katika mechi mbili zilizobaki za msimu huu.

Inasemekana kuwa kocha Roberto mancini alipokea taarifa kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Ferran Soriano kuwa anakwenda kufukuzwa kazi katika klabu hiyo kabla hajapokea simu kutoka kwa mwenyekiti wa klabu Khaldoon Al Mubarak aliyeko nchini Abu Dhabi .

Manuel Pellegrini mwenye umri wa miaka 59 sasa ameshafanya mazungumzo na Manchester city kuhusu kibarua hicho na kwamba atakuwa tayari kama city watalipa kiasi cha paundi milioni 3.3 ikiwa ni gharama ya kuvunja mkataba na malaga ikiwa ni  kipengele cha kuondoka kama ilivyo katika mkataba wake wa sasa na klabu ya malaga, na pia amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na klabu ya Barcelona ili aweze kuwa kocha wa klabu hiyo katika kipindi hiki ambacho kocha mkuu Tito Vilanova akiwa katika matibabu ya kansa.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed