KOCHA WA CHELSEA JOSE MOURINHO
Kocha wa chelsea Jose Mourinho amekasirika juu ya mchezaji Romelu Lukaku ambaye mtandao wa Sportsmail unathibisha kwamba mchezaji huyo aliomba kuondoka Chelsea baada ya kukosa kufunga mkwaju wa penati katika mchezo wa kombe la UEFA dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Siku moja baada ya Cheslea kufungwa mabao 5-4 kwa mikwaju ya Penati Romelu Lukaku aliomba kuondoka Cheslea baada ya kujiona kwamba hataweza kupambana na Fernando Torres, Demba Ba na Samuel Eto’o katika kupigania namba katika kikosi cha Chelsea uamuzi ambao kocha wa Cheslea Jose Mourinho aliukataa lakini siku tatu baadaye kocha huyo alimruhusu Lukaku kujiunga na Everton kwa mkopo na ameweza kufunga mabao saba mpaka sasa tofauti na Torres, ba na Etoo ambao wana magoli manne tu kati yao.
Mourinho alimshambulia Lukaku alipotakiwa kujibu tuhuma kutoka kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 wa ubelgiji ambaye alimlaumu kocha huyo kutokuwa na mawasiliano naye tangu aondoke kwa mkopo katika klabu hiyo.

ROMELO LUKAKU
Akimwongelea mchezaji huyo Mourinho amesema Lukaku ni kijana mdogo sana ambaye anapenda kuongea lakini kitu kimoja tu ameshindwa kuongea ni kwa nini aliamua kwenda kwa mkopo katika klabu ya Everton na hicho ni kitu cha msingi sana ambacho anapaswa kukiongea.
Mara ya mwisho nilipoongea naye nilimuuliza kwa nini hutaki kusema ukweli kwa nini haupo katika klabu ya chelsea kwa sasa. Kuna vitu katika maisha ambavyo hatutaki watu wengine wavifahamu na kuvifanya kuwa siri mioyoni mwetu lakini kuna wakati alifunga goli na kutamka kuwa nina uhakika Jose Mourinho ameona hii kwa nini aliniacha nikaondoka? alisema Mourinho.
Jose Mourinho amegoma kabisa kufafanua kuhusu suala hilo na kuendelea kusisitiza kwamba uamuzi wa kumwacha aondoke ulikuwa ni uamuzi wa ghafla sana kwa sababu mpaka dakika za mwisho mchezaji Demba ba ndiye alikuwa mbioni kutua katika klabu ya Arsenal ambayo ilikuwa inamhitaji sana mchezaji huyo lakini haikuwa tayari kutoa kiasi cha paundi milioni mbili kama ada ya uhamisho ya mchezaji huyo.
Wakati Lukaku alipoomba kuondoka ndipo klabu ikabadilisha mipango yake na kuhitisha ofa kutoka katika klabu mbalimbali zilizoonyesha nia ya kumsaji ndipo walipojitokeza Everton na West brom ambao walikuwa na nia ya kumnyakua mchezaji huyo ambaye alisajiliwa na Cheslea akitokea katika klabu ya Anderlecht ya Ubelgiji mwaka 2011.
Baada ya mipango kukamilika ndipo klabu ya Chelsea ikaamua kumwacha Lukaku aondoke kwenda Everton uku ikimwacha Ba kuendelea kukipiga katika klabu hiyo.
Maendeleo ya mchezaji huyo katika klabu ya Everton ni mazuri na yatafanya kuwe na uwezekano wa kuendelea kukipiga katika klabu ya chelsea ambayo mchezaji huyo ana mkataba nayo mpaka mwaka 2016
ROMELO LUKAKU AKIONYESHA UFUNDI WA KUCHEZA NA MPIRA
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed