Monday, December 16, 2013

BREAKING NEWS: ANDRE VILAS BOAS ATIMULIWA UKOCHA TOTTENHAM HOTSPURS BAADA YA KIPIGO CHA BAO 5-0 KUTOKA KWA LIVERPOOL

NJE: ANDRE VILAS BOAS AMETIMULIWA RASMI UKOCHA TOTTENHAM BAADA YA KIPIGO CHA JANA CHA BAO 5-0 KUTOKA KWA LIVERPOOL
NJE NDANI: KOCHA WA TOTTENHAM ALIYETIMULIWA LEO ANDRE VILAS BOAS ALITUA KATIKA KLABU HIYO KUCHUKUA MIKOBA YA HARRY REDKNAP MWAKA 2012
Andre Villas Boas ametimuliwa kuinoa klabu ya Tottenham hotspurs leo baada ya kipigo cha bao 5-0 ilichokipata Tottenham kutoka kwa liverpool pambano lililopigwa hapo jana katika uwanja wa white hart lane.

Kocha huyo kutoka nchini ureno alikuwa katika wakati mgumu sana katika klabu hiyo kwa wiki kadhaa tangu alipokubali kipigo cha bao 6-0 kutoka kwa klabu ya Manchester city katika uwanja wa Etihad lakini aliweza kujifariji kwa kupata ushindi alipocheza na Fulham na pambano aliloshinda dhidi ya Sunderland.

Lakini kipigo cha jana jumapili cha bao 5-0 kimehitimisha safari yake ya mwaka mmoja katika klabu hiyo na kufanya kocha huyo awe ametimuliwa mara ya pili mfululizo ndani ya miaka miwili baada ya awali kutimuliwa katika klabu ya Chelsea.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo ilisomeka kama ifuatavyo: klabu inatangaza kwamba makubaliano yamefikiwa na kocha mkuu Andre Villas Boas kutimuliwa kazi katika klabu hii. uhamuzi huu ni wamaridhiano ya pande zote na kwa manufaa ya pande zote mbili, tunamtakia Andre Villas Boas mafanikio uko aendako. mwisho wa kunukuu

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed