Wednesday, December 18, 2013

CAPITAL ONE CUP: SUNDERLAND YAMALIZANA NA MOURINHO YAIGONGA CHELSEA BAO 2-1

MKOREA KI SUNG AKIPIGA MPIRA KUIPATIA SUNDERLAND BAO LA PILI
KI SUNG AKIVUA JEZI KUSHANGILIA BAADA YA KUIPATIA SUNDERLAND BAO LA PILI
FRANK LAMPARD AKIGOMBEA MPIRA NA MABEKI WA TIMU YA SUNDERLAND
FABIO BORIN AKIIFUNGIA SUNDERLAND BAO LA KWANZA
Amazing: Sunderland couldn't believe their eyes after Borini put the ball in
RAHA YA USHINDI:FABIO BORINI AKISHANGILIA BAADA YA KUIFUNGIA SUNDERLAND BAO LA KWANZA
Timu ya soka ya Chelsea imetupwa nje ya mashindano ya Capital one Cup baada ya kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa klabu ya Sunderland katika pambano kali na la kusisimua lililopigwa hapo jana usiku.

Mpaka dakika ya 87 Timu ya Chelsea ilikuwa inaongoza kwa bao moja la kujifunga la Sunderland lililowekwa nyavuni na Cattermolle katika dakika ya 46 kabla ya mchezaji Fabio Borrini kusawazisha katika dakika ya 88 ya mchezo na kufanya pambano kumalizika kwa bao 1-1.

Pambano lilikwenda katika dakika za nyongeza na ndipo sunderland walipofanikiwa kupata bao la ushindi katika dakika ya 118 ya mchezo na kuwatupa nje Chelsea katika mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed