BRYAN OVIEDO AKIIFUNGIA EVERTON BAO DHIDI YA MANCHESTER UNITED HAPO JANA
BRYAN AKIPONGEZWA BAADA YA KUFUNGA BAO
LUKAKU AKIMPONGEZA OVIEDO BAADA YA BAO
WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED KUTOKA KUSHOTO-NEMANJA VIDIC NA ANTONIO VALENCIA WAKIWA NA HUZUNI BAADA YA FILIMBI YA MWISHO
Jahazi la timu ya Manchester united linazidi kwenda mrama baada ya hapo jana kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa timu ngumu ya Everton inayonolewa na kocha Roberto Martinez.
Goli la ushindi la Everton lilifungwa na Bryan Oviedo katika dakika ya 85 ya mchezo na kuwaacha hoi mashetani wekundu wa Old Trafford.
Mlolongo wa matokeo mabovu ya Manchester united yanaiweka klabu hiyo katika wakati mgumu katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka.
Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Tottenham katika uwanja wa Whitehart lane mwishoni mwa wiki iliyopita Manchester united imeendelea kupata matokeo mabovu na yasiyoridhisha baada ya kujikuta ikipata kipigo kutoka kwa everton katika uwanja wa Old Trafford.
Kipigo hicho ni cha nne kwa msimu huu na cha nne kwa kocha mpya David moyes ambaye amechukua mikoba iliyoachwa wazi na kocha aliyestaafu Sir Alex ferguson.
Matokeo hayo yanaifanya Manchester united ishike nafasi ya tisa kwa kuwa na pointi 22 katika michezo 14 ambayo imecheza mpaka sasa uku ikiwa nyuma kwa pointi 12 kwa Vinara wa ligi hiyo Arsenal wenye pointi 34 katika michezo 14.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed