
MCHEZAJI BORA WA MWAKA: LUIS SUAREZ AKIWA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA YA FOOTBALL SUPPORTERS FEDERATION AKIWA NA MKEWE SOFIA

LUIS SUAREZ AKIWA NA TUZO YAKE
Luis Suarez ametajwa kama mchezaji bora wa mwaka wa shirikisho na wanaosaidia mpira wa miguu nchini uingereza hapo jana katika hafla ya otoaji wa tuzo hizo.
Miezi mitano iliyopita baada ya Arsenal kutangaza dau la paundi milioni 40 kwa ajili ya kumnyakua mchezaji huyo kutoka uruguay hatimaye Suarez amepata tuzo katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa Emirates unaomilikiwa na klabu ya Arsenal.
Ni tuzo ya pekee kwa mchezaji wa Liverpool ambaye aliwazidi kura wachezaji wengine ambao walikuwa wanawania tuzo hiyo wakiwemo Leighton Baines, Christian Benteke, Juan Mata, Robin van Persie na Pablo Zabaleta ambapo watu 500,000 walimpigia kura Luis Suarez katika tuzo hiyo.
Luis Suarez ambaye alipokea tuzo katika uwanja wa Emirates amesema mwaka uliopita ulikuwa mwaka wa mafanikio sana kwake kwa upande wa soka na kuendelea kusisitiza kwamba tuzo hiyo siyo kwa ajili yake pekee bali ni kwa ajili ya wachezaji wote katika klabu ya Liverpool, uongozi na watu wote wanaosapoti klabu ya Liverpool.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed