Wednesday, December 04, 2013

YAYA TOURE ASHINDA TUZO YA MWAKA YA BBC YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA





YAYA TOURE AKIWA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA BBC WA AFRIKA

YAYA TOURE KATIKA HARAKATI ZAKE UWANJANI
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Ivory coast na klabu ya Manchester city ya Uingereza Yaya Habib Toure ametajwa kama mchezaji bora wa BBC kwa mwaka 2013.

Mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo amewahi kuchaguliwa mara tano kuwania tuzo hiyo lakini hakuwahi kushinda lakini safari hii ameweza kushinda akiwaacha wachezaji wengine wanne kama kiungo wa Chelsea Mikel John Obi, Victor moses wa Liverpool, Pierre-Emerick Aubameyang wa Borussia Dortmund na Mchezaji wa Rennes Jonathan Petroipa.

Mchezaji huyo akiongea na BBC amesema amewahi kushindania tuzo hiyo kwa mara tano mfululizo lakini hakuwahi kushinda na hatimaye mwaka huu amefanikiwa kushinda ni kitu kizuri na cha kushangaza sana, nina furaha sana kwa sababu ni mashabiki ndiyo wameamua kunipa tuzo hiyo kwa hiyo ninashukuru sana.

Katika kuwania tuzo hiyo wachezaji wote watano waliwekwa mbele ya wataalamu 44 wa soka kutoka afrika ambao walikuwa wakimchambua kila mchezaji kulingana na vigezo vilivyowekwa wakiangalia zaidi uwezo binafsi wa mchezaji uwanjani, kucheza kitimu, kucheza kwa kujali wengine hasa katika kutoa maamuzi.

Baada ya kukamilika kwa zoezi hilo mashabiki wa soka barani afrika walipewa nafasi ya kuchagua mchezaji bora kwa kutakiwa kupiga kura katika mtandao wa BBC na kuweza kumchagua mchezaji wanayeona ni bora na anastahili kushinda tuzo hiyo.

Pamoja na kukosa kikombe akiwa na Man city katika msimu wa 2012/2013 yaya toure amewajibika vizuri akiwa chini ya kocha Muitaliano Roberto Mancini na sasa chini ya kocha Manuel Pelegrini sababu zilizomfanya aweze kuwa juu ya wachezaji wenzake katika kuwania tuzo hizo.

Yaya Toure ameongeza kusema ni mafaniko makubwa sana kwa soka la afrika hasa katika kipindi hiki kuliko vipindi vingine vyote kwa kuwa na wachezaji wengi na wenye vipaji vya hali ya juu kabisa na kuwataja baadhi kama Aubameyang, Pitroipa, Mikel, Moses, Salomon Kalou, Gervinho na wengine wengi pia nadhani soka la kiafrika linazidi kukua na hiyo ina maana kubwa sana kwetu waafrika alimalizia Yaya Toure
WACHEZAJI WENGINE WALIOWAHI KUSHINDA TUZO HIYO NI KAMA IFUATAVYO

2012 - Christopher Katongo (Zambia and Henan Construction)


2011 - Andre 'Dede' Ayew (Marseille & Ghana)


2010 - Asamoah Gyan (Sunderland & Ghana)


2009 - Didier Drogba (Chelsea & Ivory Coast)


2008 - Mohamed Aboutrika (Al Ahly & Egypt)


2007 - Emmanuel Adebayor (Arsenal & Togo)


2006 - Michael Essien (Chelsea & Ghana)


2005 - Mohamed Barakat (Al Ahly & Egypt)


2004 - Jay Jay Okocha (Bolton & Nigeria)


2003 - Jay Jay Okocha (Bolton & Nigeria)


2002 - El Hadji Diouf (Liverpool & Senegal)


2001 - Sammy Kuffour (Bayern Munich & Ghana)


2000 - Patrick Mboma (Parma & Cameroon)








No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed