Friday, January 10, 2014

LUIS SUAREZ NA KOCHA WA MANCHESTER CITY MANUEL PELEGRIN WASHINDA TUZO YA MCHEZAJI NA KOCHA BORA WA MWEZI DECEMBA

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Luis Suarez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi desemba wa ligi kuu ya soka ya nchini uingereza baada ya kufanikiwa kufunga magoli 10 na kuweza kuisaidia kwa muda klabu yake ya liverpool kukaa katika kiti cha uongozi wa ligi hiyo ngumu duniani

Wachezaji wote wa liverpool kwa pamoja waliweza kufanya vizuri katika mapambano yao waliyocheza dhidi ya Norwich wakiweza kufunga magoli mawili,na ushindi wa magoli mawili dhidi ya westham united, tottenham na cardiff na kuweza kuishuhudia klabu hiyo ikikamata usukani wa ligi hiyo kwa muda katika kipindi cha sikukuu ya krismas.

Kocha wa klabu ya Manchester city Manuel Pellegrin ameweza kujinyakulia tuzo ya kocha bora wa mwezi Desemba kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea katika klabu ya Malaga ya uhispania
Mshambuliaji wa klabu ya liverpool Luis Suarez akiwa na Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Desemba

Kocha wa Manchester city Manuel Pellegrin akiwa na Tuzo ya kocha bora wa Mwezi Desemba


        REKODI ZA KUIS SUAREZ MWEZI DESEMBA
TAREHEWAPINZANIMATOKEOMAGOLI
Dec 1Hull (A)3-10
Dec 4Norwich (H)5-14
Dec 7 West Ham (H)4-12
Dec 15 Spurs (A)0-52
Dec 21 Cardiff (H)3-12
Dec 26Man City (A)2-10
Dec 29 Chelsea (H)2-10
      REKODI ZA MANUEL PELLEGRIN KWA MWEZI DESEMBA
     TAREHEWAPINZANIMATOKEO
December 1Swansea (H)3-0
December 4 West Brom
(A)
2-3
December 7 Southampton (A)1-1
December 14 Arsenal (H)6-3
December 21 Fulham (A)2-4
December 26Liverpool
(H)
2-1
December 29 Crystal Palace (H)1-0


No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed