
JUAN MATA KULIA AKISAINI MKATABA WA KUICHEZEA MANCHESTER UNITED UKU AKIWA NA KOCHA WA TIMU HIYO DAVID MOYES

SHABIKI WA MANCHESTER UNITED AKIWA NA JEZI YA MCHEZAJI MPYA WA KLABU HIYO JUAN MATA

JUAN MATA AKIWASILI KATIKA VIWANKA VYA MAZOEZI VYA KLABU YA MANCHESTER VYA CARRINGTON

JUAN MATA NDANI YA JEZI YA MANCHESTER UNITED
Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amesmea kuwa ulikuwa ni 'uamuzi mgumu' kwake kumwachia mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Uhispania Juan Mata kujiunga na wapinzani wao katika ligi kuu ya England Manchester United.
Mata mwenye umri wa miaka, 25, ameweka rekodi ya uhamisho katika klabu ya Man United baada ya kuuzwa na Chelsea kwa kititia kirefu cha pauni milioni 37.1.
Akizungumza na BBC Mourinho amesema:
" Haya ni maamuzi ambaye mkufunzi anapaswa kufanya, lakini kwangu ilikuwa vigumu. Ningependa kuendelea kumwona katika kikosi changu bila shaka,""Lakini kuwa katika hali hii kwa mchezaji ni vigumu. Anastahili kuachiwa milango wazi katika Chelsea. Napenda kuwaona watu wakiwa na raha. Nasikitika sikuweza kumfurahisha katika kikosi hiki - nasikitika sana kwa hilo, lakini najenga kikosi changu nikizingatia mchezaji Oscar ambaye anacheza katika nafasi ya 10," anasema mzee Mourinho.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed