Friday, February 07, 2014

BREAKING NEWS:NEMANJA VIDIC ATANGAZA RASMI KUONDOKA MANCHESTER UNITED

NEMANJA VIDIC KUSHOTO WA MANCHESTER UNITED AMETANGAZA KUIACHA KLABU HIYO MWISHONI MWA MSIMU HUU
KOCHA WA MANCHESTER UNITED DAVID MOYES (KUSHOTO) ATALAZIMIKA KUFIKIRIA MIPANGO YA MSIMU UJAO WA LIGI KUU ENGLAND BILA YA MLINZI NEMANJA VIDIC (KULIA)
NEMANJA VIDIC AKIONEKANA KAMA ANAWAAGA MASHABIKI WA UNITED ALIPOKUWA AKITOKA KATIKA VIWANJA VYA MAZOEZI VYA KLABU HIYO
KOCHA WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED SIR ALEX FERGUSON(KUSHOTO) ALIMSAJILI NEMANJA VIDIC KUTOKA KLABU YA SPARTAK MOSCOW MWAKA 2006

Mlinzi wa kati wa klabu ya Manchester united Nemanja Vidic ametangaza rasmi kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu baada ya kukataa kufanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya klabuni hapo.

Kocha mkuu wa klabu hiyo David moyes alikuwa na mipango ya kuendelea kumtumia mlinzi huyo lakini mchezaji huyo ambaye mkataba wake uko mbioni kumalizika ameonyesha nia ya kuondoka klabuni hapo baada ya kuitumikia mklabu hiyo kwa miaka 9.

Akiwa na klabu ya Manchester United Vidic aliweza kushinda vikombe 15 baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea katika klabu ya Spartak Moscow ya nchini urusi kwa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 7 mwaka 2006 na kufanikiwa pia kuwa mchezaji imara sana katika safu ya ulinzi ya Manchester united chini ya kocha aliyestaafu Sir Alex Ferguson.

Katika taarifa iliyotolewa na mtandao wa klabu hiyo wa manutd.com vidic alikaririwa akisema kwamba ni mwaka wangu wa mwisho katika mkataba wangu klabuni hapa na nimekuwa na maisha mazuri klabuni hapa kwa miaka 9

Muda wote niliokaa hapa nitauchukulia kama muda mzuri wa kukumbukwa katika maisha yangu yote ya soka, sikuwahi kufikiria kama ningeweza kushinda mataji 15 nikiwa mahali hapa pia siwezi kuusahau usiku mzuri katikam historia uliojitokeza katika jiji la Moscow tulipotwaa ubingwa wa UEFA mbele ya mashabiki wa chelsea. Kumbukumbu zote hizi zitabaki katika maisha yangu yote.

Hata hivyo nitaondoka mwishoni mwa msimu huu ili niweze kuangalia changamoto mpya katika maisha ya soka mahali na sehemu nyingine.

Siwezi kuendelea kukaa england kwa sababu nilikuwa na klabu ambayo nilikuwa na mapenzi nayo ya dhati kabisa na nilikuwa na bahati kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika klabu hii kwa miaka 9, ninafikiria kuondoka mahali hapa na nitaangalia kilicho bora kwangu na kwa familia yangu.

Kwa sasa ninaangalia zaidi maendeleo yangu katika klabu ya manchester united na kufanya yote yanayowezekana kuweza kuisaidia klabu kufanya vizuri mpaka mwisho wa msimu.

Alipoulizwa kuhusu mustakabali wa nemanja vidic kocha wa manchester united David moyes alisema sifahamu chochote kuhusu mkataba wa sasa wa Nemanja vidic, bado sijautazama upya mkataba wake nina uhakika mkurugenzi mkuu na klabu wanafahamu kuhusu hilo.

Timu nyingi barani ulaya zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi timu hizo ni za junentus,Inter milan na Ac milan zote za italia,Monaco ya Ufaransa pamoja na Galatasaray ya nchini uturuki.

Vidic alianza kuwa kapteni wa klabu ya Manchester united katika mbio za taji la 20 chini ya kocha Sir Alex Ferguson na mpaka sasa amecheza mechi 390 na united akifunga magoli 35 katika mashindano yote, amefanikiwa kunyakua mataji matano ya ligi kuu uingereza,kombe moja la ubingwa barani ulaya,mataji matatu ya kombe la ligi, mataji mataji ya ngao ya jamii pamoja na kombe moja la klabu ya dunia.

NEMANJA VIDIC FACTFILE

1981: Born October 21 in Titovo Uzice in Yugoslavia.
1996: After impressing in youth football he is signed up by Red Star Belgrade.
2000-01: Spends his first season in the professional ranks on loan at Spartak Subotica.
2001-02: Returns to Belgrade and helps them to win the Yugoslav Cup.
2002: October 12 - Makes his international debut for Serbia and Montenegro against Italy in a Euro 2004 qualifier.
2004: Under his captaincy, Red Star win the Serbia and Montenegro league and cup double.
July - Moves to Russian Premier League side Spartak Moscow for an undisclosed fee.
2005: December 25 - Manchester United confirm Vidic has agreed to join them in an estimated £7million deal. Makes his debut in a Carling Cup semi-final second-leg victory over Blackburn.
2006: Misses out on playing at the World Cup through suspension and injury having been part of a back four that conceded just one goal in 10 qualifying matches.
2006-07: Helps United regain the Premier League title after forming an excellent defensive partnership with Rio Ferdinand. Also plays in FA Cup final defeat to Chelsea at Wembley.
2007: November 8 - Signs a two-year contract extension to keep him at Old Trafford until 2012.
2008: Helps United to claim their second straight league title and win the Champions League against Chelsea in Moscow.
2009: Plays in every game as Edwin van der Sar sets world record of 1,311 minutes without conceding a goal. Wins a third consecutive championship title. Introduced as a second-half substitute as United defeat Tottenham in the Carling Cup final. Completes full 90 minutes in Champions League final defeat to Barcelona in Rome.
October 29 - Sent off in a 2-0 defeat against Liverpool. It marks the third consecutive match against the Merseysiders in which he has been dismissed.
2010: Wins second consecutive League Cup winners' medal as United beat Aston Villa at Wembley. Plays in Serbia's World Cup campaign as they exit in the first round despite beating Germany 1-0.
August - Signs four-year contract extension. Named United skipper.
2011: Leads United to another championship but part of team beaten by Barcelona in the Champions League final at Wembley.
December - Ruptures cruciate ligaments in Champions League defeat to Basle. Ruled out for remainder of season, having already missed eight weeks with a calf injury.
2012: Returns for opening-day defeat at Everton but comeback lasts just five games before forced to undergo a second operation, keeping him out for three months.
2013: Captain United to the league title - the fifth of his time at Old Trafford.
2014: Sent off in final minute of Premier League defeat at Chelsea - the sixth red card of his United career, two of which came against the Stamford Bridge outfit and three against Liverpool.
2014: February - confirms he will leave Manchester United at end of the season.
 


No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed