Kipigo hicho ni cha nane kwa Man united msimu huu katika ligi kuu inayoendelea nchini england na kitamfanya Kocha wa klabu hiyo david moyes kuchanganyikiwa endapo atapata vipigo vingine zaidi.
ifuatayo ni orodha ya misimu iliyopita na nafasi ambazo manchester united ilikamata baada ya michezo 24.

WAYNE ROONEY KATIKATI AKIWA HAAMINI BAADA YA KUPATA KIPIGO CHA KWANZA KUTOKA KWA STOKE CITY TANGU MWAKA 1984

HALI MBAYA: DAVID MOYES AMEKUWA NA MATOKEO MABAYA TANGU ACHUKUE TIMU KUTOKA KWA SIR ALEX FERGUSON
NI REKODI NGAPI ZISIZOHITAJIKA AMBAZO MOYES ATAZIVUNJA MSIMU HUU?
Manchester united imeshapoteza michezo nane msimu huu katika ligi kuu ya nchini uingereza ambayo ni idadi ya michezo kwa ujumla ambayo ilipoteza katika msimu wa 2001/02 na 2003/04 na kumaliza nafasi ya tatu katika misimu yote miwili.
Manchester united imeshapoteza michezo minne katika uwanja wa nyumbani wa Old Trafford mpaka sasa na endapo manchester united itapoteza michezo mingine mitatu itaivunja rekodi yake ya kufungwa michezo sita nyumbani ambayo ilifungwa katika msimu wa 2001/02
Msimu uliopita katika utawala wa Sir Alex Ferguson Manchester united iliweza kupata pointi nyingi zaidi katika michezo 24 kuliko misimu mingine yote iliyopita.Msimu huu chini ya David Moyes hali ni mbaya sana katika michezo 24

KIWANGO KIBOVU: MSIMU HUU HALI MBAYA KULIKO VIPINDI VINGINE VYOTE
Mara ya mwisho Manchester united ilipoteza michezo 10 katika msimu mzima wa ligi na hiyo ilikuwa ni mwaka 1990/91 na walimaliza ligi wakiwa nafsi ya sita.
Rekodi ya klabu ya kufungwa katika michezo 38 ilijumuisha kufungwa michezo 16 katika msimu wa 1989/90 Manchester united ilimaliza nafasi ya 13 katika msimu huo ikiwa ni msimu wa tatu kamili chini ya utawala wa Sir Alex Ferguson kama kocha wa Manchester United.
Ikiwa imepoteza michezo mitatu mfululizo(dhidi ya Spurs, Swansea na Sunderland) kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2001,mara ya mwisho kufungwa mfululizo ilikuwa ni mwaka 1961 baada ya kupata vipigo mfululizo kutoka kwa Birmingham, Arsenal, Bolton na Sheffield Wednesday

WACHEZAJI WA ARSENAL WAKISHANGILIA USHINDI WA BAO 3-1 DHIDI YA UNITED HII ILIKUWA MSIMU WA 1990/91
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed