Wednesday, March 26, 2014

KIPIGO CHA BAO 3-0 CHA MAN UNITED KUTOKA KWA MAN CITY CHAIMALIZA MANCHESTER UNITED

EDIN DZEKO AKISHANGILIA BAADA YA KUIPATIA MAN CITY BAO LA KWANZA
WACHEZAJI WA MAN CITY WAKIMPONGEZA DZEKO BAADA YA KUFUNGA BAO LA KWANZA
EDIN DZEKO AKIFUNGA BAO LA PILI
YAYA TOURE AKIIFUNGIA CITY BAO LA TATU

Matumaini ya klabu ya Manchester United kuingia katika timu nne za juu katika ligi kuu ya nchini yametoweka jana usiku baada ya kujikuta wakichapwa mabao 3-0 na Manchester city katika uwanja wa Oldtrafford na kupoteza matumaini kabisa.

Iliwachukua Manchester city dakika moja kuweza kupata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Edin Dzeko dakika moja baada ya mchezo kuanza na kuweza kuwachanganya kabisa wachezaji wa Manchester united.

Manchester united ambao wiki iliyopita waliweza kuonyesha mpira safi walipofanikiwa kuingia robo fainali ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kuifunga Olympiakos ya ugiriki kwa magoli 3-0 pia pambano safi la ushindi wa bao 2-0 kutoka kwa Westham united walijaribu kupambana kwa nguvu bila mafanikio yoyote mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Manchester city walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa nguvu uku kila mmoja akijaribu kutumia mbinu kuweza kumfunga mwenzake lakini walikuwa ni Manchester city tena walioweza kupata bao la pili katika dakika ya 56 kwa bao safi lililofungwa na Edin Dzeko baada ya kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Samir Nasri.

Mambo yalizidi kuwa magumu kwa Manchester united baada ya kujikuta wakifungwa bao la tatu na kiungo mshambuliaji wa Manchester city Yaya Toure katika dakika ya 90+2 na hivyo Man city kutoka Mbele kwa Ushindi wa bao 3-0.

Kwa matokeo hayo Manchester united wamejikuta katika wakati mgumu na kupoteza matumaini ya kuingia katika timu nne za juu ( Top Four) baada ya kucheza michezo 31 na kuwa na pointi 51 wakiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo kwa sasa chelsea kwa pointi 18 na pointi 15 nyuma ya Mahasimu wao wa jiji la Manchester, Manchester city.

Kama Manchester united itashindwa kuingia katika timu nne za juu itashindwa kushiriki katika mashindano yajayo ya klabu bingwa barani ulaya na hivyo kujikuta wakiangukia katika mashindano ya UEFA EUROPA league.

Ili kuweza kushiriki katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya msimu ujao Manchester united wanatakiwa kushinda ubingwa wa UEFA CHAMPIONS league ili waweze kushiriki mashindano hayo kama bingwa mtetezi.

VIKOSI

Man Utd: De Gea 6, Da Silva 5, Jones 5.5, Ferdinand 5, Evra 6, Fellaini 4.5 (Valencia 66, 6), Carrick 5.5, Cleverley 6 (Kagawa 46, 5.5), Mata 6, Rooney 7, Welbeck 6.5 (Hernandez 77, 6).
Subs not used: Lindegaard, Young, Fletcher, Buttner.
Booked: Welbeck, Fellaini.
Man City: Hart 7, Zabaleta 6, Kompany 7, Demichelis 6.5, Clichy 6, Toure 7, Fernandinho 7.5, Jesus Navas 6.5 (Garcia 68, 6), Silva 8, Nasri 6.5 (Milner 74, 6), Dzeko 7, (Negredo 79, 5.5).
Subs not used: Lescott, Kolarov, Pantilimon, Jovetic.
Booked: Kompany, Fernandinho.
Goals: Dzeko 1, 56, Toure 90+2. 
Referee: Michael Oliver 6 


No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed