Friday, March 28, 2014

SERENA WILLIAMS AMSHINDA MARIA SHARAPOVA NA KUTINGA FAINALI ZA SONY OPEN

SERENA WILLIAMS AKISHANGILIA BAADA YA KUMSHINDA MARIA SHARAPOVA NA KUTINGA FAINALI YA NANE YA SONY OPEN
MARIA SHARAPOVA AKIPAGAWA BAADA YA KUTOLEWA KATIKA MASHINDANO YA SONY OPEN NA SERENA WILLIAMS
Serena Williams alifanikiwa kushinda michezo mitano kutoka 4-1 chini katika seti ya kwanza na kufanikiwa kushinda set 6-4 6-3.

Haikuwa kazi rahisi alisema mwanadada huyo ambaye anashika nafasi ya kwanza kwa ubora kwa upande wa wanawake duniani,maria sharapova alicheza vizuri sana na nilijitahidi kukaa mchezoni na kuhakikisha ninashinda pambano hili kwa kupiga mipira mingi zaidi.

Kwa ushindi huo mwanadada huyo anatazamiwa kucheza katika pambano la fainali ambapo atakutana na mwanadada kutoka slovakia Dominika Cibulkova au Mchina Li Na.

Ni ushindi mzuri na wa kushangaza kwangu alisema williams baada ya kufanikiwa kutinga katika fainali yake ya tisa.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed