Tuesday, April 08, 2014

CRISTIANO RONALDO AOKOA MAISHA YA MTOTO ALIYEZIMIA KWA MIEZI MITATU


KIJANA DAVID AKIWA NA CRISTIANO RONALDO

KIJANA DAVID AKIKARIBISHWA KATIKA MJIJI LA MADRID.

WAKATI WA MIUJIZA: DAVID AKIAMKA KUTOKA KATIKA KOMA KWA MATANGAZO YA RADIO WAKATI CRISTIANO RONALDO ALIPOFUNGA BAO BAO LA TATU(HAT-TRICK) KATIKA PAMBANO LA KUFUZU KWA KOMBE LA DUNIA DHIDI YA SWEDEN MWEZI NOVEMBA 

DAVID AKIKABIDHIWA JEZI YA REAL MADRID NA CRISTIANO RONALDO

DAVID AKIWA NA FAMILIA YAKE ILIYOSAFIRI KUTOKA POLAND HADI MADRID BAADA YA KUPATA MWALIKO KUTOKA KWA CRISTIANO RONALDO

Bao lililofungwa na Cristiano Ronaldo katika mechi ya kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia dhidi ya Sweden limesaidia kuokoa maisha ya mtoto David Pawlaczyk aliyezimia kwa muda wa miezi mitatu na wawili hao walifanikiwa kukutana kwa furaha baada ya pambano la ushindi wa Real madrid dhidi ya Dortmund wiki iliyopita katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya.

David Pawlaczyk alipata ajali mbaya baada ya kugongwa na gari akiwa anendesha baiskeli yake na kupata majeraha mengi nya ndani ya mwili mwezi august mwaka jana.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 14 alikimbizwa hospitali lakini aliweza kukaa katika koma kwa muda wa miezi mitatu, taarifa kutoka gazeti la poland la Fakt. 

Wazazi wa kijana huyo waliambiwa kuwa tiba ya sauti ni tumaini lililobaki kuweza kumtoa kijana wao katika koma na waliambia wanatakiwa kutumia sauti ambazo zinafahamika sana na kijana wao.

David ni shabiki kubwa wa Real madrid na Cristiano ronaldo ni mchezaji anayempenda sana na wazazi wake wamekuwa wakimsikilizisha matangazo mengi ya radio yanayohusu real madrid na namna mtangazaji anvyotangaza magoli yanayofungwa na Cristiano Ronaldo.

Wakati Cristiano Ronaldo alipofunga goli katika pambano dhidi ya sweden mwezi novemba kijana Davidi alikuwa anasikiliza matangazo hayo na sauti hiyo ya matangazo ndiyo iliyoweza kumtoa kijana huyo kutoka katika koma ya miezi mitatu

Vyombo vya habari vya Poland viliweza kutangaza taarifa hiyo ambayo ilimfikia Cristiano Ronaldo na hivyo kuamua kumwalika kijana huyo na familia yake waweze kuungana naye katika jiji la Madrid ambapo Real madrid walikuwa wakipambana na dortmund.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed