Wednesday, April 02, 2014

SERENA WILLIAMS ASHINDA MASHINDANO YA WAZI YA SONY BAADA YA KUMSHINDA LI NA WA CHINA


MWANADADA SERENA WILLIAMS AKIWA NA KOMBE LA UBINGWA BAADA YA KUMSHINDA LI NA 
LI NA KUSHOTO AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA SERENA WILLIAMS BAADA YA PAMBANO LAO
MWANADADA SERENA AKIRUKA JUU KWA FURAHA BAADA YA KUFANIKIWA KUMSHINDA LINA


SERENA WILLIAMS AKIRUDISHA MPIRA ULIOPIGWA NA MWANADADA LI NA
MWANADADA LI NA AKIPAMBANA KWA NGUVU NA SERENA WILLIAMS
Mwanadada Serena Williams ameweka rekodi ya kushinda taji la saba baada ya kumshinda mwanadada Li na kwa seti 7-5, 6-1 katika mashindano ya wazi ya Sony yaliyofanyika katika jiji la miami nchini Marekani.

Serena Williams ameivuka rekodi ya mataji sita aliyokuwa akiishikilia pamoja na Andre Agassi. Lakini katika pambano la juzi mwanadada huyo alionekana kuanza pambano hilo akiwa mchovu na kufanya makosa mengi ambayo yalikuwa yanatishia ushindi wake baada ya kujikuta akiwa nyuma kwa seti 5-2

Kipindi fulani nikiwa mchezoni niliona kama sina kitu cha kupoteza alisema serena niliweza kupumzika na kila nilipopumzika nilijihisi furaha, Li na aliweza kusevu seti 5-4 kabla ya serena kurudi kwa nguvu na kuweza kushinda kwa mipira ya kurudisha.

Serena Williams alihitaji dakika 21 kuweza kumaliza seti, mchezo wa mwisho katika seti hiyo ulikuwa na makosa sita lakini serena williams aliweza kushinda kwa mipira ya nguvu ambayo Li alishindwa kuhimili.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed