Friday, June 27, 2014

MANCHESTER UNITED YACHUKUA WAWILI KWA MPIGO

Manchester united imetoa kiasi cha Paundi milioni 58.8 kuwanasa wachezaji Luke shaw kutoka southampton na Ander Herera kutoka klabu ya Atletico Bilbao katika harakati zake za kutaka kurejesha makali katika ligi kuu ya nchini uingereza ambayo inatazamiwa kuanza kupigwa kuanzia mwezi agosti 2014.

Manchester united itakamilisha uhamisho wa paundi milioni 30 kwa mlinzi wa kushoto wa timu ya taifa ya uingereza Luke shaw leo ijumaa masaa 24 baada ya kutoa kitita cha paundi milioni 28.8 kwa mchezaji wa nafasi ya kiungo kutoka Atletico Bilbao ya nchini uhispania Ander Herera.

Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward ametenga kiasi cha paundi milioni 60 ili kuweza kusaini wachezaji haraka iwezekanavyo ili kuepuka makosa yaliyojitokeza msimu uliopita na kuendelea kusisitiza kwamba usajili bado unaendelea.

ANDER HERERA AKIWA NA JEZI YA MANCHESTER UNITED

LUKE SHAW NAMBA 23 AKIWA KATIKA HARAKATI ZAKE UWANJANI
Ingawa klabu ya Southampton ilikuwa inataka kiasi cha paundi milioni 40 kwa ajili ya Luke shaw wamekubali ofa ya paundi milioni 30 na hivyo kumruhusu mchezaji huyo kujiunga na united ambapo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya yake leo ijumaa tayari kuingia mkataba mpya wa miaka mitano na united.

HERERA KULIA AKIWA UWANJANI NA JEZI ZA BILBAO
ANDER HERERA KUSHOTO AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BOBBY CHARTON
 

DONDOO KUHUSU WACHEZAJI HAO

ANDER HERRERA, MIDFIELDER, AGE 24
2008-2009: Zaragoza B (10 apps, 2 gls)
2009-2011: Zaragoza (82, 6)
2011-2014: Athletic Bilbao (94, 7)
2014-NOW: Manchester United
LUKE SHAW, LEFT-BACK, AGE 18
2012-2014: Southampton (60 apps, 0 gls)
2014-NOW: England (3 caps, 0 gls)

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed