Monday, June 09, 2014

ZIMESALIA SIKU NNE KABLA YA KOMBE LA DUNIA
Je wafahamu kuwa....
Bingwa wa Kombe la Dunia 2014 atashinda dola milioni 35.
Kiasi hicho ni kikubwa zaidi kuliko kiasi walichoshinda Spain, mabingwa wa Kombe la Dunia miaka minne iliyopita. Spain walipata dola milioni 31. Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valcke amesema mshindi wa pili atapewa dola milioni 25.
Mshindi wa tatu atapatiwa dola milioni 22, na wa nne milioni 20.
Kila nchi itakayoingia katika raundi ya mtoano imehakikishiwa kupewa dola zisozopungua milioni 8.
Kiasi cha fedha zilizopo kwa nchi na vilabu vilivyotoa wachezaji ni dola milioni 576. Mwaka 2010 fedha hizo zilikuwa dola milioni 420.
Nchi na vilabu zitapatiwa jumla ya dola milioni 100 kwa kuwezesha wachezajikupatikana na kuweza kushiriki.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed