
RANGI MPYA: ADAM LALLANA AKIWA NA JEZI MPYA YA KLABU YA LIVERPOOL BAADA YA KUKAMILISHA UHAMISHO KUTOKA SOUTHAMPTON

AKIWA KATIKA CHUMBA CHA KUBADILISHIA NGUO


ADAM LALLANA AKIFANYIWA VIPIMO VYA AFYA YAKE
Adam Lallana ametangazwa rasmi kama mchezaji mpya wa klabu ya Liverpool baada ya kukamilisha uhamisho wa paundi milioni 23 kutua klabuni hapo kutoka katika klabu ya Southampton.
Mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya Uingereza ametimiza ndoto zake za kuitumikia klabu ya Liverpool baada ya kuonekana katika picha akiwa na jezi nyekundu za klabu ya Liverpool katika viwanja wa Melwood ambako Liverpool inafanyia mazoezi baada ya kukamilisha vipimo vya afya yake wikiendi iliyopita.
Kucheleweshwa kwa mikataba yake kulifanya klabu ya Liverpool kuchelewa kumtangaza rasmi mchezaji huyo lakini baada ya kumalizana na Southampton mambo yote yapo sawa na usajili wake kukamilika.
Akiwa katika Klabu yake mpya ya Liverpool Lallana atavaa jezi namba 20,baada ya kukamilisha uhamisho wake Lallana ameuambia mtandao wa klabu ya Liverpool kwamba anajisikia furaha kufungua ukurasa mpya katika klabu ya Liverpool na ana hamu kubwa sana ya kuanza kuichezea klabu hiyo.
Ni matumaini yangu kuwa nitakuwa sawa haraka iwezekanavyo na kuweza kujitoa kwa moyo wangu wote kuitumikia klabu hii katika kipindi chote nitakachokuwa hapa kwa sababu nipo hapa kwa ajili ya mafanikio.
'
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed