Wednesday, September 03, 2014

ALVARO NEGREDO ALIPOTAMBULISHWA RASMI KUWA MCHEZAJI MPYA WA VALENCIA

KUREJEA LA LIGA: ALVARO NEGREDO AMEKAMILISHA UHAMISHO WA KUICHEZEA VALENCIA KWA MKOPO KUTOKA KLABU YA MANCHESTER CITY YA UINGEREZA
DILI KUBWA: MANCHESTER INATAJIA KUVUNA KITITA CHA PAUNDI MILIONI 23.8 KWA MAUZO YA MCHEZAJI HUYO MSIMU UJAO
NEGREDO AKIPITA MBELE YA MASHABIKI WA KLABU YA VALENCIA BAADA YA KUTAMBULISHWA RASMI KWA MASHABIKI HAO
NEGREDO AKIWA NDANI YA UZI MPYA WA KLABU YA VALENCIA
Alvaro Negredo ametambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa klabu ya Valencia baada ya kukamilisha uhamisho wa mkopo kutoka klabu ya Manchester city ya uingereza.

Mchezaji huyo alitambulishwa rasmi mbele ya mashabiki wenye shauku ya kumwona waliokuja kwa wingi katika uwanja wa Mestalla hapo jana jioni na anatarajiwa kuanza kuichezea klabu hiyo katika pambano la Valencia dhidi ya Espanyol tarehe 14 septemba.

Negredo aliweza kuandika barua kwa mashabiki wa Manchester city katika mtandao wake wa Twitter akielezea shukrani zake kwa mashabiki hao kwa upendo na kumuunga mkono alipokuwa katika klabu hiyo mwaka mmoja uliopita.

Mchezaji huyo wa uhispania ambaye aliigharimu Manchester city kiasi cha paundi milioni 20 alipojiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Sevila ya uhispania mwaka mmoja uliopita aliweza kufunga magoli 12 katika mapambano 20 aliyoichezea klabu hiyo lakini alijikuta akipata wakati mgumu kuweza kucheza katika kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa wachezaji wa kiwango cha hali ya juu katika klabu hiyo na hivyo kuweza kuanza katika mapambano matatu tu baada ya januari.

Negredo aliweza kufunga magoli 23 katika mapambano yote aliyoichezea klabu ya manchester city na kufanikiwa kunyakua taji la ubingwa wa ligu kuu ya uingereza pia kunyakua kombe la capital one.

Katika barua yake aliyowaandikia mashabiki wa manchester city negredo anasema: napenda kuishukuru klabu kwa kunifanya kuwa mchezaji mkubwa na kunifanya mimi na familia yangu kujisikia tupo nyumbani wakati wote nilipokuwa uingereza.

Manchester city ni klabu ambayo itakaa moyoni mwangu maisha yangu yote, ilinipa nafasi ya kuweza kucheza katika ligi ngumu ya uingereza na ni jambo kubwa sana kwangu kuweza kushinda kikombe cha ligi kuu england pamoja na kikombe cha capital one na kuweza kufunga magoli 23 kwangu ni kama ndoto iliyokuwa kweli.

Negredo amejiunga kwa mkopo klabu ya Valencia na klabu hiyo ipo mbioni kutoa kitita cha paundi milioni 23.8 kuweza kumnyakua mchezaji huyo moja kwa moja.




No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed