Friday, September 12, 2014

DIEGO COSTA ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI AUGUST


Diego Costa is the Barclays Premier League Player of the Month after some fine performances for Chelsea

DIEGO COSTA AKIWA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA KWA MWEZI AUGUST BAADA YA KUWA NA MWANZO MZURI KATIKA KIKOSI CHA CHELSEA


KOCHA GARY MONK WA SWANSEA AKIWA NA TUZO YA KOCHA BORA WA MWEZI AUGUST BAADA YA KUIWEZESHA SWANSEA KUFANYA VIZURI KATIKA MWANZO WA LIGI HIYO KWA KUWEZA KUSHINDA MICHEZO YOTE MITATU
Diego Costa amefanikiwa kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi august baada ya kuiwezesha klabu yake ya chelsea kufanya vizuri katika mapambano yake ya mwanzo wa msimu wa ligi kuu ya nchini uingereza.

Mchezaji huyo mbrazil mwenye uraia wa uhispania alifunga magoli manne katika michezo mitatu ambayo ameitumikia klabu hiyo ya darajani baada ya kusajiliwa akitokea katika klabu ya Atletico Madrid ya uhispania.

Diego Costa anaungana na kocha wa klabu ya Swansea Gary Monk ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa mwezi august baada ya kuiwezesha klabu ya Swansea kushinda michezo mitatu katika michezo mitatu iliyocheza msimu huu ikiwemo pambano lake la kufungua dimba msimu huu dhidi ya Manchester United katika dimba la Oldtrafford.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed