Tuesday, October 21, 2014

MATOKEO MECHI YA JANA USIKU: WEST BROM 2 MANCHESTER UNITED 2



DELAY BLIND AKISHANGILIA BAADA YA KUIPATIA UNITED BAO LA PILI LA KUSAWAZISHA KATIKA PAMBANO LA JANA USIKU
SAIDO BERAHINO AKIMPITA RAPHAEL NA KUPIGA MPIRA ULIOIPATIA WEST BROM BAO LA PILI
BERAHINO AKIIFUNGIA WEST BAO LA PILI
BERAHINO AKISHANGILIA BAADA YA KUIPATIA BROM BAO LA PILI
ANGEL DI MARIA AKIONYESHA UFUNDI WAKE KATIKA PAMBANO LA JANA USIKU
STEPHANE SESSEGNON AKIPIGA MPIRA NA KUIFUNGIA WEST BROM BAO LA KWANZA
SESSEGNON AKISHANGILIA BAO LA KWANZA KWA WEST BROM
FELLAIN AKIINGIA KUTOKA KATIKA BENCHI NA KUIPATIA UNITED BAO LA KWANZA NA LA KUSAWAZISHA
FELLAINI AKIUNGANA NA WACHEZAJI WENGINE WA UNITED KUSHANGILIA BAO LA KWANZA LA KUSAWAZISHA
DI MARIA AKITOKA NA NAFASI YAKE KUCHUKULIWA NA ASHLEY YOUNG

Ligi kuu ya England imeendelea jana usiku ambapo Manchester United ilijikuta ikibanwa mbavu na kushindwa kufurukuta ugenini kwa Westbromwich Albion na kutoka sare ya mabao 2-2 licha kwamba ilitawala mchezo huo.

Mchezo huo wa pekee kwa ratiba ya ligi hiyo ulishuhudiwa Man United ikishindwa kupata walau ushindi wake wa kwanza nje ya uwanja wake wa nyumbani tangu timu hiyo iwe chini ya kocha Louis Van Gaal.

Ni bao la Daley Blind katika dakika za mwisho za mchezo ambalo limeiokoa Manchester United kuzama katika mpambano huo. Awali Stephane Sessegnon wa Westbrom aliitungua United kwa bao la mapema kabla ya Marouane Fellaini aliyeingia kipindi cha pili kusawazisha muda mfupi tu baada ya kuingia uwanjani.

Mshambuliaji kijana Saido Berahino aliipatia Westbrom goli la pili ambalo lilidumu hadi pale Blind aliposawazisha na kuinusuru United na kichapo katika mtanange huo uliochezeshwa na mwamuzi Mike Dean.


VIKOSI

West Brom 4-2-3-1: Myhill 7; Wisdom 7, Dawson 7, Lescott 7, Pocognoli 6; Gardner 7, Morrison 6; Dorrans 7.5, Sessegnon 7 (Mulumbu 86), Brunt 6.5; Berahino 7.
Subs not used: Daniels, Blanco, McAuley, Gamboa, Anichebe, Ideye.
Goals: Sessegnon 8, Berahino 66 
Booked: Morrison
Manchester United 4-3-1-2: De Gea 6; Rafael 6, Jones 6, Rojo 5, Shaw 5; Herrera 5.5 (Fellaini 46, 7), Blind 6, Di Maria 7 (Young 76); Mata 6 (Falcao 72, 6); Van Persie 6, Januzaj 5.5.
Subs not used: Lindegaard, Smalling, Fletcher, Carrick
Goals: Fellaini 48, Blind 87 
Booked: Blind 
MOM: Graeme Dorrans
Referee: Mike Dean

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed