Ligi kuu ya soka nchini uingereza imefika mahali patamu hasa katika kipindi hiki cha christmas baada ya kushuhudia mapambano makali yakipigwa hapo jana katika ratiba ya kukamilisha msimu wa sikukuu ya christmas.
Siku ya jana ilishuhudia mapambano makali yakipigwa na kushuhudia matokeo mengi ambayo wengi hawakuyategemea.
Vinara wa ligi kuu nchini england Chelsea walishuka dimbani hapo jana na kupambana na Southamton ambayo msimu huu imeonyesha uhai mkubwa sana na matokeo ya pambano hilo ni sare ya bao 1-1 na kuifanya timu ya chelsea kpunguza kasi ingawa bado inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo, mabao katika pambano hilo yalifungwa na mchezaji sadio mane na lile la kusawazisha la chelsea lilifungwa na Eden Hazard aliyefanya juhudi binafsi kwa kuihadaa ngome ya southamton na kupata bao la kusawazisha.
EDEN HAZARD AKIRUKA HEWANI KUSHANGILIA BAO LAKE DHIDI YA SOUTHAMPTON
HAZARD AKIPONGEZWA
SADIO MANE AKISHANGILIA BAO ALILOFUNGA DHIDI YA CHELSEA
Nayo klabu ya Manchester united hapo jana ilitoka sare ya bila kufungana na klabu ya Tottenham huku Manchester united ikishindwa kuzitumia nafasi nyingi za wazi kuweza kujipatia matokeo mazuri
PHIL JONES AKIWA CHINI NA KUSHUHUDIA MPIRA WA KICHWA ALIOUPIGA UKITOLEWA NA KIPA HUGO LLRIS
VAN PERSIE AKIZUIWA KUFUNGA BAO KATIKA PAMBANO LA JANA
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed