
CRISTIANO RONALDO AMETAJWA KAMA MCHEZAJI BORA WA MWAKA KWA MARA YA NNE

CRISTIANO RONALDO AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MAMA YAKE MZAZI MARIA PAMOJA NA MTOTO WAKE CRISTIANO JR
Mwanasoka wa klabu ya Real Madrid na Timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amekuwa na mwaka wenye mafanikio baada ya hapo jana kutajwa kama mshindi wa tuzo ya Ballon D'or kwa mara ya nne katika hafla iliyofanyika katika jiji la Paris nchini Ufaransa.
Mchezaji huyo alipata kura 173 zilizopigwa na waandishi wa habari za michezo duniani kote na kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo huku akiwaacha nyuma wapinzani wake Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Grienzmann walioshika nafasi ya pili na ya tatu.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed