Baada ya wiki iliyopita kuifunga Transit Camp 8-0, Jana Azam FC iliifunga Tanzania Prisons 1-0 goli likifungwana Ibrahim Mwaipopo katika dakika ya 34
Mshabuliaji John Bocco ambaye alianza na Papi (Mkongo aliye kwenye majaribio na baadaye kuwapisha KipreTchetche na Gaudence Mwaikimba wote walicheza vizuri sana katika mechi hiyo licha ya kushindwa kufungakutokana na kukusa bahati
Katika mchezo wa Jana Prisons ilifanya shambulizi moja tuu, lakini Azam FC muda wote walikuwa kwenye lango la Prisons
Viungo Abdi Kassim, Jabir Aziz, Abdulhalim Humud na Ibrahim Mwaipopo walitawala sehemu ya kiungo nakuwachanganya maadui. Kila mmoja wao alipata nafasi ya kupiga mashuti golini mwa adui ingawa mipira yao ilipaaau kuokolewa na kipa wa Prisons
Katika Mchezo wa Jana Abdulhalim Humud ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo
Azam FC ilikwakilishwa na Deogratius Munishi, Ibrahim Shikanda, Aggrey Morris, Said Moradi, Erasto Nyoni/WaziriSalum, Abdulhalim Humud, Jabir Aziz/Himid Mao Abdi Kassim, Ibrahim Mwaipopo/Kipre Bolou, John Bocco/KipreTchetche, Papi/Mwaikimba
SOURCE:http://www.azamfc.co.tz
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed