MBUYU TWITE MWENYE JEZI YA NJANO AKIWA AMEONGOZANA NA VIONGOZI WA YANGA WALIOKUJA KUMPOKEA
MBUYU TWITE AKIWA NA KATIKA MKUU WA YANGA MWESIGWA SELESTIN
MASHABIKI WA YANGA
Mchezaji mpya wa kimataifa wa timu ya taifa ta Rwanda ,Mbuyu Twite amewasili leo jijini Dar kutokea nchini Rwanda tayari kujiunga na mabingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati timu ya Young Africans.
Twite aliwsali majira ya saa 10:15 kwa majira ya Afrika Mashariki kwa shirika la ndege la Rwanda Air na kupokelewa na viongozi wa Young Africans na washabiki wengi waliojitokeza kumpokea Uwanja wa ndege wa Mwl JK Nyerere.
Mara baada ya kuwasili mlango wa kutokea watu mashuhuri, Twite alipewa jezi ya Yanga yenye namba 4 mgongoni iiiliyoandikwa jina la Aden Rage, mwenyekiti wa Simba.
Umati mkubwa ulijitokeza kiasi kilichopelekea Twite kushindwa kutokea mlango wa kawaida wa kupelekea uongozi wa uwanja huo kumuongoza Twite kutokea mlango wa wageni mashuhuri.
Msafara ulianza Uwanja wa ndege wa Mwl JK Nyerere kuelekea makao makuu ya klabu, huku magari yakiwa mengi, pikipiki na wengine wakitembea kwa miguu mpaka makao makuu ya klabu.
Msafara uliendelea mpaka makao makuu ya klabu, kwa kupitia mtaa wa msimbazi ambapo wapenzi na washabiki wa simba hawakuweza kuamini macho yao mara baada ya kumuona Twite akiwa katika gari ndogo ya Yanga, na washabiki na wanachama wakiwazomea simba na kuwakejeli kwa maneno ya dhihaka. Mara baada ya kufika makao makuu ya klabu ya Yanga, mchezaji Mbuyu Twite alipanda juu ghrorofani kuwasalimia washabiki na wanachama waliojitokeza kumpokea, kisha alikabidhiwa funguo ya chumba ambacho atakua akikitumia kwa kipindi chote atakachokuwa Yanga.
Mbuyu Twite amesema anajisikia vizuri, na furaha na mwenye bahati kuja kuchezea timu ya Yanga na anawaahidi kuonyesha kiwango cha juu kipindi chake chote atakaoitumikia Young Africans, Twite kesho anatajumuika na wenzake katika mazoezi asubuhi Uwanja wa Loyola kabla ya jumamosi kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Coastal Union.
SOURCE:http://www.youngafricans.co.tz
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed