Saturday, August 04, 2012

FABRICE MUAMBA AKARIBIA KURUDI DIMBANI

FABRICE MUAMBA amethibitisha ujio wake katika soka baada ya kucheza mechi ya kujipima nguvu alipokuwa mapumzikoni jijini Dubai
Mchezaji huyo ambaye anakipiga katika klabu ya Bolton ya uingereza ameonyesha maendeleo mazuri baada ya kupona shambulio la moyo ambalo lilimpata.

Muamba mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akiendelea vizuri kutokana na shambulio la moyo lililompata mwezi march mwaka huu lakini ameweza kujiunga na wenzake na kufanya mazoezi wakati akiwa mapumzikoni mapema mwezi huu uko dubai ambapo muamba na mkewe Shauna magunda walikuwepo.

Nilikuwa katika mapumziko na kulikuwa na baadhi ya wchezaji pia katika hoteli niliyofikia,mara nikasikia wafanyakazi wa hoteli wakiandaa pambano na wageni wa hoteli hiyo nikaona ni bora nijumuike nao. Niliwaambia rafiki zangu pamoja na mpenzi wangu shauna samahani sana lakini ni lazima nishiriki pambano hili ndipo nikaingia kucheza pamoja nao. 

Nilicheza kwa dakika 25 na ilikuwa kama niko mazoezini ilikuwa safi sana nilifurahi sana, alisema Fabrice muamba.

Namshukuru sana Mungu kwa hali niliyonayo sasa, nadhani nitarudi kucheza soka muda wowote kuanzia sasa alimalizia kusema muamba

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed