Monday, August 13, 2012

KOLO TOURE AKWARUZANA NA MANCINI

KOLO TOURE-KULIA
ROBERTO MANCINI
Mwisho wa mchezaji kolo toure kuendelea kukipiga katika klabu ya Manchester city umefika baada ya jana kuonekana akitupa medali yake aliyoipata katika ushindi walioupata dhidi ya Chelsea katika ngao ya jamii kwa mashabiki katika uwanja wa villa park.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory coast mwenye umri wa maka 31 sasa aliachwa katika benchi la wachezaji wa akiba wakati mabingwa hao wa uingereza walipoichapa chelsea kwa mabao 3-2 na Kolo Toure amehusishwa na Kugombana na kocha wake Roberto Mancini baada ya kupulizwa kwa filimbi ya mwisho.

Picha mbalimbali zilizowekwa katika mtandao wa kijamii wa twitter zinamwonyesha shabiki mmoja akiwa amebeba medali inayosadikiwa kuwa ni ya Kolo Toure ambayo inasemakana aliitupa kwa mashabiki baada ya kukwaruzana na kocha wake Roberto Mancini hii ni kutokana na Gazeti la Daily Mirror

Kolo Toure aliwekwa katika benchi na nafasi yake kuchukuliwa na Stevan Savic katika mechi ya ngao ya jamii ambayo iliishuhudia Manchester city ikiwafunga chelsea ndani ya sekunde kumi kwa magoli yaliyowekwa nyavuni na Yaya Toure, Carlos Tevez na Samir Nasri.

Kolo toure ambaye amebakiza miezi 12 katika mkataba wake wa sasa na manchester city anatarajiwa kuuzwa kwa kiwango kidogo cha paundi milioni 3 ambazo zinaonekana nyingi kwa Timu za Bursarsport na Trabzonspor za uturuki ambazo zinashindwa kufikia makubaliano ya gharama hiyo.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed