Wednesday, August 01, 2012

KUTOKA AZAM FC

Ngasa akaribia kutua Simba SC... watoa ofa ya Milioni 25. Yanga waishia milioni 20
Hadi hivi sasa Ofa ya Simba ni shilingi Milioni 25 na Yanga ni Milioni 20. kutokana na hilo. Simba wapo kwenyenafasi kubwa ya kumnyakua Mrisho Ngasa. Kesho ni siku ya Mwisho. Ingawa tungependa kumuuza Mrisho NgasaYanga lakini tutampeleka kwa timu iliyotoa ofa nzuri zaidi

Lengo la Azam FC lilikuwa ni kumpeleka Mrisho kwenye timu ambayo atacheza kwa raha na amani, kutokana na yeyekuivaa na kuibusu Jezi ya Yanga siku ambayo Azam FC haikuwa na mchezo na Yanga... Azam FC inaamini kuwaYanga ilikuwa Sehemu sahihi kwa Mrisho, lakini uongozi wa Yanga umeonekana kutokuwa na haja na Mrisho nandiyo maana umeonekana kukataa kutoa ofa ya maana. Kutokana na sababu hizo Azam FC italazimikakumuuza Mrisho Ngasa Simba kwani hatuhitaji kuwa na mchezaji ambaye anafanya vitendo vya kuidharau brand yaAzam FC ambayo tunajaribu kuijenga.

Imetolewa na Utawala
Azam FC

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed