RAPPER SNOOP DOGG amejibatiza yeye mwenyewe kama mfalme wa Reggae na sasa anajiita Snoop Lion
Harakati za mwanahip hop huyo ambaye siku za karibuni amekuwa na imani za dini ya rastafarian zimekuja baada ya kufanya ziara katika miji kadhaa ya jamaica.
Mwanamuziki huyo maarufu wa hip hop mwenye umri wa miaka 40 sasa ambaye jina lake halisi ni Calvin Cordozar Broadus Jr amesema umefika wakati wa kulizika jina la Snoop dogg na kutambulisha jina lake jipya la SNOOP LION.
Sikutambua hilo mpaka nilipokwenda katika Temple ambalo mhubiri aliniuliza jina lako nani nikamjibu naitwa Snoop Dogg, alinitazama machoni na kusema wewe ni Nuru na kuanzia sasa utaitwa Lion alisema snoop dogg.
Mwanamuziki huyo mwenye itikadi ya Gangstar na anayeamini kwamba yeye ni mzaliwa mpya wa bob marley, amerekodi albamu ya reggae na moja ya nyimbo zilizopo katika album hiyo ni ''No Guns allowed''
Simba wa Judah ni dini maarufu sana ambayo inawakilisha watu wenye imani za kirastafari
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed