Friday, August 03, 2012

LUCAS MOURA KUTUA MANCHESTER UNITED KWA ADA YA UHAMISHO YA PAUNDI MIL.30

LUCAS MOURA
Manchester united iko mbioni kukamilisha usajili wa mchezaji Lucas Moura kutoka katika klabu ya Sao Paulo ya Brazil kwa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 30 baada ya kupata taarifa kwamba Paris st. Germain wako mbioni pia katika harakati za kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19.

Kocha wa manchester united Sir Alex ferguson amemshuhudia mchezaji huyo akiichezea timu ya taifa ya Brazili dhidi ya New zealand katika mashindano ya Olimpiki yanayoendelea katika jiji la London nchini Uingereza na anatarajia kufanya mazungumzo ya kukamilisha uhamisho huo ifakapo Alhamisi ijayo.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed