Friday, August 03, 2012

NURI SAHIN AKARIBIA KUTUA ARSENAL KWA MKOPO

NURI SAHIN
Kocha mkuu wa klabu ya real madrid Jose mourinho ametoa baraka zake kwa mchezaji wake kinda kutoka Uturuki Nuri sahin kuweza kwenda katika klabu ya arsenal kwa mkopo.

Jose Mourinho amesema kwamba hawezi kumhakikishia mchezaji huyo wa kimataifa wa uturuki namba katika kikosi cha kwanza cha Timu ya real madrid ambayo kumejaa wachezaji wengi wenye vipaji.

Mchezaji huyo amabye alijiunga na timu ya real madrid kwa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 8/ kutoka katika klabu ya Borussia Dortmund ambako aliweza kuisaidia timu hiyo kunyakua mataji na pia kuweza kuibuka kama mchezaji bora kwa mwaka huo.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed