ROBIN VAN PERSIE
LUCAS MOURA
SIR ALEX FERGUSON
Manchester united imekubali kutoa kitita cha paundi milioni 30 kumsajili mchezaji kinda wa timu ya sao paulo ya brazil Lucas moura na kocha mkuu wa manchester united Sir alex ferguson ana matumaini ya kutumia kiasi kilichobaki cha paundi milioni 20 kuweza kukamilisha uhamisho wa Robin Van persie kutoka katika klabu ya Arsenal mwishoni mwa wiki hii.
Lucas Moura atafanyiwa vipimo vya afya yake leo katika jijji la manchester tayari kwa uhamisho wake wa kutua Old trafford baada ya Mbrazil huyo kuiwakilisha Timu yake ya taifa katika ushindi wa lioupata katika pambano la Olimpiki dhidi ya Honduras ambapo mbrazil huyo alianzia katika benchi.
Wakati manchester united wakiwa safarini kuelekea Norway hapo jana kupambana na valencia katika maandalizi ya msimu ujao wa ligi ya uingereza kocha mkuu wa klabu hiyo Sir alex ferguson amebaki ili kuweza kukamilisha usajili wa lucas moura na Robin van persie wakati zikiwa zimebaki siku 14 kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili na kocha huyo anahakikisha kwamba mchezaji Robin van persie anavaa jezi ya united katika msimu ujao wa ligi.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed