
Katika kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya mzunguko wa pili na mashindano ya Afrika Azam FC imefanya usajili wawachezaji nane wapya katika kipindi hiki cha dirisha dogo
Azam FC ambayo ilikuwa na wachezaji wanne wa kimataifa kufiatia George Odhiambo kuondolewa mapemakutokana na utovu wa nidhamu pia iliwapunguza wachezaji Ibrahim Shikanda na Joseph Owino na hivyo kuwa nanafasi tatu za kimataifa
Azam FC imejaza nafasi hizo kwa kuwasajili Jockins Atudo, beki wa kati wa Harambee Stars na klabu ya Tusker FC,Kiungo mshambuliaji wa Harambee Stars na Sofapaka Humphrey Mieno pamoja na mshambualiaji na mchezajibora wa mashindano ya CECAFA Challenge Cup Brian Umony.
Pia Azam FC imemsajili kinda anayeshika nafasi ya pili kwa kufunga magoli ligi kuu akiwa na magoli sita nyuma yaKipre Tchetche na Didier Kavumbangu wenye magoli nane kila mmoja Seif Rashid Abdallah toka Ruvu Shooting Stars
Kama hiyo haitoshi Azam FC ambayo ilikuwa na uwakilishi mkubwa zaidi kwenye mashindano ya CECAFAChallenge Cup mwaka huu kwa kuwa na wachezaji 11, imemewarudisha walinzi Malika Ndeule na Omary Mtakiwaliocheza katika vilabu vya African Lyon na Mtibwa Sugar katika mzunguko wa kwanza.
Katika kuimarisha safu yake ya ulinzi pia imemsajili mlinzi wa kati wa Tanzania Prisons David Mwantika. Na kumsajilikwa mkopo winga wa Simba Uhuru Selemani.
Usajili huu umesimamiwa na mwalimu Stewart Hall mwenyewe ambaye anaamini maboresho haya yatakiongezeanguvu kikosi cha Azam FC katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza januari 20.
Azam FC ipo jijini Kinshasa DRC ikijiandaa na mzunguko wa pili na mashindani ya kimataifa kwa kusaka uzoefu wakucheza nje ya nchi na imeshacheza michezo miwili na timu za Dragons and FK Sharks ambapo ilitoka sare 1-1mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa pili 0-2.
Azam FC inatarajia kurejea nchini December 26 ambapo itaelekea visiwani Zanzibar moja kwa moja kushirikimashindano ya Mapinduzi Cup ambayo inayashikilia.
SOURCE:http://www.azamfc.co.tz
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed