
Kikosi cha Young Africans Sports Club
Kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi yake leo katika Uwanja wa Bora eneo la Mabatini Kijitonyama kujiandaa na safari ya ziara ya mafunzo nchini Uturuki wiki ijayo ambako pia itatumia nafasi hiyo kufanya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na kombe la Kagame.
Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga mholanzi Ernie Brandts amesema anafurahishwa na mwenendo wa timu yake, kwani toka wameanza mazoezi ni wiki ya tatu sasa na anawaona wachezaji wako katika hali nzuri, kimwili, kifikra na kiakli, na kuamini ziara ya Uturuki itamsadia kuwaweka vizuri zaidi.
Mapema mwezi uliopita mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb alitangaza program ya timu kwa kipindi hichi cha mwezi disemba, timu itakwenda kuweka kambi nchini Uturuki kwa kipindi cha wiki mbili ambapo ikiwa huko inatarajiwa kupata michezo miwili hadi mitatu ya kirafiki kulingana na ratiba watakayokuwa wamepewa na wenyeji wao.
Safari ya Uturuki itajumuisha wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa pamoja na benchi la ufundi.
Yanga ilianza mazoezi tarehe 26 Novemba 2012 chini ya kocha Brandts na wachezaji wote wameendelea na programu ya kocha ambapo jana asubuhi walifanya mazoezi ya ufukweni katika eneo la Coco Beach.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed