Wednesday, December 19, 2012

CLAUDIO RANIERI AMTAKA DAVID BECKHAM KUTUA MONACO


 
DAVID BECKHAM
Kocha wa klabu ya Monaco Claudio Ranieri anamkaribisha David beckham kwa mikono miwili kutua katika klabu ya Monaco inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Ufaransa maarufu kama Ligue 2 akiwa na uhakika kwamba nahodha huyo wa zamani wa uingereza atakuwa msaada kwa kila idara katika klabu hiyo.

Ranieri ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa klabu hiyo ameweza kuisaidia klabu hiyo kufanya vizuri katika michezo yake ya daraja la kwanza ya ufaransa.

Timu hiyo ya ufaransa imekuwa ikihusishwa na kumsajili David beckham baada ya kumaliza mkataba wake wa sasa na klabu ya marekani ya LA Galaxy na kocha wa klabu hiyo amesema kwamba anavutiwa sana na mchezaji huyo na kwamba angependa kuona mchezaji huyo akijiunga na klabu hiyo.

Akiongea na gazeti maarufu la ufaransa Le Parisien Ranieri alisema David Beckham atakuwa msaada sana katika maendeleo ya klabu hii kwa kuweza kuwatia hamasa wachezaji wadogo wa klabu hii na hivyo kuwajengea kujihamini katika kila hatua wanayopiga na kuendelea kusisiza kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 sasa anaendelea vizuri na ni mwenye uzoefu sana katika soka la kisasa.

Akiongea kutoka klabuni hapo bilionea mmiliki wa klabu hiyo Dimitry Rybolovlev amesema klabu hiyo ina pesa za kutosha kuweza kumlipa mchezaji huyo ikiwa ni moja ya malengo ya klabu hiyo kuweza kurejea katika ligi ya juu ya nchi hiyi maarufu kama League 1

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed