Wednesday, December 19, 2012

M'BAYE NIANG YUKO MBIONI KUTUA ARSENAL



Timu ya soka ya Arsenal imeweka ofa mezani kwa mchezaji wa timu ya taifa ya ufaransa na caen ya ufaransa M'baye Nianga.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 sasa ameshafanya majaribio na klabu hiyo ya London na Arsenal imethibisha kwamba mchezaji huyo yuko mbioni kutua katika klabu hiyo inayotumia uwanja wa Emirates kwa mkataba wa muda mrefu.

Hata hivyo klabu ya arsenal siyo pekee ambayo imetuma ofa kwa ajili ya mchezaji huyo kuna klabu mbili za uingereza ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo na klabu moja kutoka italia ambayo pia imeonyesha nia ya kumnyakua mchezaji huyo

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed