
LUIS NANI AKIWA NA BAADHI YA WATOTO WA CHINI YA MIAKA 10 WA TIMU YA WATFORD
Picha ikimwonyesha mchezaji wa manchester united luis nani akiwa katika viwanja vya michezo vya timu ya arsenal imeleta uvumi kwamba mchezaji huyo yuko mbioni kutimkia katika klabu ya arsenal.
Habari kutoka gazeti la sporstmail zimethibitisha sababu ya mchezaji huyo kuonekana mahali hapo.
Mchezaji huyo wa manchester united alikuwa karibu na mlango wa kuingilia chuo cha mafunzo cha watford(uwanja wa zamani wa mazoezi wa arsenal) wakati picha ikipigwa siku ya jumapili na hakuwa hapo kwa sababu ya kuonana na arsene wenger kama ilivyoripotiwa bali alikuwa maeneo hayo kumwangalia mtoto wa mchumba wake akiwa anacheza mpira katika timu ya watoto chini ya miaka 10 ya watford.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed